Dini yako sio muhimu sana


salimkabora

salimkabora

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2012
Messages
2,449
Points
1,225
salimkabora

salimkabora

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2012
2,449 1,225
Kuna watu wako tayari kuuwa, kutukana, kukebehi, nk ktk harakati za kulinda dini yao lakini hawako tayari kuilinda dini kwa kuwa mfano wa maadili mema au chemchem na kisima cha amani na hekima ambako wengine wanaweza kuiga na kuchota maarifa.

Imani ni kile unachokiishi.

Unachokiamini huenda kikawa ndio dini yako. Dini inakuwa imani pale inapokugeuza na kukufanya uishi kama vile dini yako inavyofundisha. Hapa ndipo penye utata wa kutisha. Mtu anaamini katika dini inayopinga ushirikina, uganga, usihiri na mizingu ya aina zote. Hata hivyo haachi kwenda kwa hao masangoma. Mtu dini yake inakataza zinaa, lakini yeye ndiye kinara wa hayo, na isitoshe huenda ni kiongozi katika ibada za dini yake.
Anaamini vingine na anaishi vingine. Matokeo ya hayo ni kwamba unachokiishi ndio mbegu unayopanda na ndio itakayoota katika maisha yako. Ukiomba kulingana na sala za dini yako hufanikiwi kwakuwa maombi ya matendo yako yameshatangulia na kusomeka kama maombi muhimu zaidi juu ya uhai wako.
Unaomba uzima unapokea mauti, Unaomba salama unapokea ajali, unaomba afya unapokea maradhi. Hakuna kukoma kwa hayo hadi ubadilike. Sasa kama hivi ndivyo, uko wapi sasa umuhimu wa dini?
 

Forum statistics

Threads 1,285,255
Members 494,502
Posts 30,855,575
Top