Mungu yupi ambaye hana dini?
Neno Mungu ni KIWAKILISHI cha NGUVU KUU iliyopo kila mahali (Omnipresent) kwa wakati mmoja (Omnipotent) na ya kwamba kila kinachoonekana na kisichoonekana vyote vimebeba NGUVU KUU kwa levels tofauti tofauti.
NGUVU KUU (THE SUPER CONSCIOUS ENERGY) ni nishati ambayo kila kitu kimetokana nayo.
Inafahamika kwamba "energy can neither be created nor destroyed, but can be transformed into another form"
Ndio maana watu wa dini hii SUPER CONSCIOUS ENERGY wenyewe wanaiita Mungu; kwa sababu ya kutokuwa na mwanzo wala mwisho na kuwa ndani ya kila kitu na kuwepo kila mahali.
Hilo ndilo neno sahihi kwao na linalowapa amani pale wanapotaka kuiongelea hii Nguvu Kuu!
Nguvu Kuu ni 'tata sana' (very complex) kiasi kwamba bila kuitafiti kitaalam huwezi kuielewa kamwe kwa tabia zake na hasa hii tabia ya kubadilika-badilika.
Uwa inabadilika katika maumbo (forms) na hali (state) tofauti tofauti.
Kulingana na Kanuni ya polarity, energy ina direction mbili za transformation (mabadiliko)
Mabadiliko yaliyosababisha 'consciousness' na
mabadiliko yaliyosababisha 'matter'.
•Matter ni maada; yaani kitu chochote chenye uzito na kinachochukua nafasi ni maada na hiyo ni kulingana na Physics form one!
'Consciousness' hatukuisoma tulipokuwa Form One, hivyo tunaweza kuitafsiri kama ile hali ya asili ya kitu; yaani kitu kimejikuta kipo hivyo kilivyo na hakijui kwa nini kipo hivyo!
Hata binadamu alipojikuta yupo vile alivyo alichanganyikiwa.
Kwa sababu ya huko kuchanganyikiwa akaona 'isiwe tabu' acha aseme chanzo chake ni kiumbe tata (complicated being) na akakipa jina yeye mwenyewe.
Jina Mungu (God, Allah etc) ni majina ambayo yametokana na binadamu kuirejelea Nguvu Kuu.
Sasa kwa lugha nyepesi tunaweza kusema consciousness ni ufahamu (may be); hivyo maada (matter) na ufahamu (consciousness) vyote ni energy, si tunaenda sawa?
Yaani vyote ni product of energy katika law of polarity. Upande huu kuna 'matter' na upande ule kuna 'consciousness'.
Vyote viwili vinategemeana na vyote vina- react!
Ngoja kwanza niongelee natural Kingdoms ambazo tunaweza kuziita asili ya uumbaji. Zipo kingdoms nne:
1. Mineral Kingdom
2. Plant Kingdom
3. Animal Kingdom
4. Humanoid Kingdom
Consciousness inapoingia kwenye minerals, mfano kwenye 'mawe', inachofanya ni kuifanya ardhi na vyote vilivyomo (minerals nk) kuwa na hali fulani ya ufahamu, wenyewe mnaita 'roho'!
Ni sawa tu, kwa sababu roho pia ni energy.
Hivyo tunakubaliana sasa kwamba energy in the form of consciousness ikiwa ndani ya jiwe, mineral au udongo, inaachilia uhai ndani yake.
Kwa nje na kwa mwonekano wake ni jiwe lakini kwa ndani (uhalisia wake) ni 'Living Stone' yaani jiwe lenye uhai au tuseme roho ndani yake!
Hii level ya uhai tunasema ipo kwenye dimensions za chini kabisa kwa sababu jiwe halina 'brain' kuweza kuchakata na kuchanganua mambo, lakini ndani yake kuna uhai ambao tunaweza kuuita 'cosmic sub consciousness'.
Baada ya hapo (after some times) ile consciousness, yaani ule ufahamu unaingia kwenye level ya pili ya Plant Kingdom na kuji-store mle. Ndio maana tunasema mimea na miti ya kila aina inasikia na kuelewa kila kitu ingawa haiwezi kusema kwa sauti kama wanyama na binadamu, lakini ina roho ndani yake na hii tunaweza kuiita 'collective sub consciousness'.
Yaani ufahamu wa mimea ni zaidi ya ufahamu wa mawe; mimea ina some intelligence kuliko mawe!
Baada ya muda fulani ile consciousness inapoendelea 'ku- develop' inaingia kwenye level ya 3, kwenye animal Kingdom level.
Wanyama wa aina mbalimbali wana roho au ufahamu mkubwa kuliko mimea na mawe.
Huu ufahamu unaitwa Sub consciousness; yaani unaweza kuongea na wanyama kwa ishara wakakuelewa kwa urahisi zaidi kuliko miti na mawe!
Hao wanyama pamoja na kuwa kwenye sub consciousness level, bado wanatofautiana ufahamu kwenye hiyo level, sawa na binadamu.
Licha ya binadamu sote kuwa kwenye level moja ya ufahamu, bado tunatofautiana kiufahamu!
Energy ikitoka hapo kwenye animal kingdom inakwenda kwenye level of consciousness ambayo ndio hii human Kingdom!
Hiyo ni energy evolution, from lowest level to the highest!
Binadamu ndiye kiumbe pekee chenye uwezo wa ku-access sub consciousness na super consciousness chenyewe kikiwa kwenye consciousness level.
Binadamu anaweza kuchukua nguvu (energies/ power/ upako) kutoka kwenye first level of consciousness mpaka kwenye highest level of consciousness!
Maana yake ni binadamu peke yake kati ya kingdoms zote NNE ndiye mwenye ubongo unaoweza ku- access hizo energies zote.
Binadamu anaweza kuamua kitu chochote kiwe Mungu kwake na kikawa.
Akiamua jiwe liwe Mungu wake na lifanye Miujiza inakuwa.
Akiamua mti fulani awe Mungu wake au akaamua Ng'ombe, Mbuzi, Chui, Nyoka, Samaki nk wawe Mungu kwake, inakuwa; kwa sababu ya ubongo ambao una NGUVU (energies) za kutosha za asili ya uumbaji iliyosababisha kila kitu kuwepo.
Mtu akiamua Mungu wa Israeli, Yesu au Maria awe Mungu wake inakuwa.
A
Mwingine akiamua Allah awe Mungu wake au Muhammad awe mtume wake inakuwa; kwa sababu brain ikiamua chochote kiwe na nguvu inakuwa!
Ndio maana kwenye dini zote na imani zote duniani kila moja hudai ndiyo sahihi na iliyo bora zaidi kuliko zingine.
Ndiyo tabia ya dini, kwa sababu mtu anaona kila akiomba kwa Jina la Mungu wake anapata majibu!
Kwa watu waliokwishavuka levels za mambo ya dini kwao kila kitu ni sawa tu maana hakuna binadamu aliye bora zaidi ya mwingine mbele za NGUVU KUU!
NB
Hii ni tafsiri yangu kuhusu Mungu sio lazima ukubaliane na mimi