Dini si Ucha Mungu

Dini si Ucha Mungu

African Believer

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
436
Reaction score
428
Kuna watu wanahisi pindi wakiwa wafuasi wa dini fulani basi hapo hapo wanakua wacha Mungu.

Ukweli ni kuwa dini ni mfumo wenye kanuni, sheria pamoja na taratibu ambazo zikifuatwa sawasawa zitamwongoza mtu kuwa mcha Mungu na si vinginevyo.

Kwa mfano, utakuta mtu anazini, anaiba, anasengenya, anatukana, anazusha uongo, ana ubinafsi, uchoyo, chuki pamoja na mengine mengi yanayofanana na hayo lakini anadai yeye ni mwanadini na kupitia hilo yeye ataiona pepo kwa kuwa tu mfuasi wa dini fulani.

Ucha Mungu ni utu wema na hutoka rohoni kwa mtu, na hudhihirika kupitia; upendo, umoja, uaminifu, kujitoa kwa ajili ya wengine, Kufunga na kuomba kwa moyo mkunjufu wenye unyenyekevu mkuu.
 
Naomba unipe elimu zaidi kuhusu hili, mtu anaweza akawa ana mawasiliano na Mungu pasipo Kuwa na dini????
Ndiyo
Mtu aweza kuwa na mawasiliano na Mungu pasipokuwa na dini.

Hebu fikiria kuhusu Ukristo na Uilsamu ambazo ni dini mbili kubwa. Dini zote mbili zilianza kuwepo na kupata wafuasi katikati ya (700 B.C mpaka 700 A D) Mkristo akiwa ni mfuasi wa Yesu Kristo na Mwislamu akifuata mafundisho ya mtume Muhammad. Na kuna makumi elfu ya wacha Mungu waliishi kabla yao.

Lakini kabla ya ujio wa hao mitume wawili maandiko mbalimbali yanatuonesha kulikua na watu wengi wacha Mungu kabla ya kusimikwa kwa itikadi mbili kuu yaani ile ya Ukristo na Uislamu achilia mbali Wayahudi pamoja na Wabudha.

Kumbuka pia swala la ibada na maombi ni la mtu binafsi na Mungu, hivyo kufanikiwa kwake kutategemea na matendo yako pamoja na dhamira yako ni si kwa kundi uliloko.
 
Ni tangu nilipojua kumbe dhambi ya kudanganya ni sawa tu na muuaji, mmbakaji, jambazi n.k

Mbinguni tutafika wachache sana iwapo na mimi nikitubu kesho.
 
Naomba unipe elimu zaidi kuhusu hili, mtu anaweza akawa ana mawasiliano na Mungu pasipo Kuwa na dini????

Dini si Mungu na Mungu si dini....dini zimewekwa tu ili sie wanadamu tuwe na kanuni ya kufuata na imani ya kumjuwa Mungu. Rudia katika asili yetu ya zamani kabla ya waarab na wazungu kuja kuturubuni na hizi dini zao. Uhitaji kuwa muislam au mkristu ili umjuwe ama kuwa karibu na Mungu, Mungu ni Imani na matendo yake. Kabla ya kuja waarab na wazungu mababu zetu waliishi kwa amani tena ya bila kuwa na ubaguzi, ila baada ya kuletewa hizi dini zisizo na manufaa kwetu ndipo tumeaanza ujinga wa kubaguana kuwa huyu ni muislam na yule mkristu, ni ujinga mtupu. Angalieni hata huko kwao, mpaka leo waarab na wayahudi wanapigana vita wanataka kutushirikisha sie tuungane na upande mmoja, hatuhitaji hizi dini.....zilishalaaniwa toka kitambo.
 
Umenena vyema sana, mababu zetu walitenda kwa uadilifu pasipo kuwa na dini. Mungu yupo kila mahali na zama zote watu wake walimtambua pasipo kuwa na hiki kinachoitwa dini.
 
Back
Top Bottom