Did we just gave presodency to s1 irrelevant? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Did we just gave presodency to s1 irrelevant?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Geza Ulole, Dec 16, 2009.

 1. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,067
  Likes Received: 3,998
  Trophy Points: 280
  Ninaposoma news kama hizi kila siku huwa najiuliza, Is Tanzania deserving this? Did we just gave presidency to s1 who does not honour his authority we entrusted and bestowed upon him! How can we avoid this nuissance? This is getting to my nerves now! Pretty disgusting and wanna know who Kikwete serves? and why the heck is he still in power? Is there a need for Tanzania to remain Independent if our minds are not liberated at all! If we have a bunch of goons ruining this country the way they are pleased? Where is the Mighty Parliament? Do they know a vote of no confedence? Do they know serving the interest of a nation? Then why there has not been a vote of no confidence now and since independence? Where is the love for our mother land? probably most of Tanzanians keep confusing Patriotism with Nationalism! Is there a need to be Nationalistic while the country is being crippled through plundering our resources and through breaking into BOT and becoming an overnight billionair!? Open your eyes lost Men and Women, we wont get there this way!! Wipe off the tears of your generation to come cause they dont deserve to get what they are about to with our own current disgraced makings! By the way just to remind you s1 is being authenticated on how to rule while at power by a renowned scholar! This happens only in Tanzania! I am humbled to be a Tanzanian, get your butts upss acts together you lost people !!!!!! fight for accountability  Prof Shivji asema Rais Kikwete ana mamlaka kisheria kuwabana mafisadi
  [​IMG]*WENGINE WAMTAKA WAZIRI CHIKAWE AACHE KUKURUPUKA

  Na Sadick Mtulya

  SIKU moja baada ya Waziri wa Sheria na Katiba Mathias Chikawe kusema Rais Jakaya Kikwete hawezi kutumia mamlaka yake kuwabana mafisadi, baadhi ya wanasheria nchini, akiwamo Profesa Issa Shivji, wamepinga kauli hiyo kwa kusema sio kweli.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana wanasheria hao walisema rais anaweza kuwabana mafisadi kwa kutumia mamlaka yake ndani ya chama na serikali.

  Profesa Issa Shivji alisema Rais Kikwete anaweza kupambana na watuhumiwa wa ufisadi kwa kuwavua madaraka walionayo katika chama au serikali.


  Gwiji hilo la Sheria na Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, alisema kama watuhumiwa watakuwa watumishi wa serikali au watendaji katika mashirika ya umma, rais anaweza kuwawajibisha kwa kutumia sheria na kanuni za utumishi wa umma.


  “Kumwajibisha mtuhumiwa sio iwe kumpeleka mahakamani, unaweza kuchukua hatua za awali ikiwemo kumvua nyadhifa zote. Kama ni mwanasiasa au mtumishi katika serikali na mashirika ya umma, unaweza kumwajibisha kwa mujibu wa sheria za umma," alisema Profesa Shivji.


  Alisisitiza “Kusema Rais Kikwete hana uwezo wa kuwabana mafisadi sio kweli na Watanzania wanatakiwa kuelewa hivyo kwamba rais anaweza.”

  Kauli ya Profesa Shivji iliungwa mkono na Profesa Abdallah Safari, aliyetia ngumu akisema sheria za nchi ikiwemo ya utawala, inampa uwezo na mamlaka rais kupambana na vitendo vya ufisadi ndani ya serikali yake na hata katika chama chake.

  “Rais kukasimu mamlaka yake kwa Takukuru (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ) na kwa DPP haimaanishi kwamba sasa yeye hana uwezo wa kupambana na watu wanaojihusisha na ufisadi. Bado anao,” alisema Profesa Safari.

  Alifafanua kwamba, Rais Kikwete anayewajibika katika kupambana na ufisadi kwa kuwa yeye ndiye anayewajibika moja kwa moja kwa wananchi wa Tanzania.

  Profesa Safari ambaye aliwahi kuwa mtumishi wa umma, alisema rais anatoa madaraka kwa vyombo vingine ili kusaidiwa, lakini bado ndiye anayewajibika kwa kuhakikisha vyombo hivyo vinawajibika ipasavyo.

  "Suala hili ni kama vile baba anamwambia mtoto wake nisaidie jambo hili na kama akishindwa au akifanikiwa na yeye anawajibika katika hayo, sasa kusema hana uwezo wa kupambana na mafisadi sio kweli na kauli hiyo inapotosha jamii," alisema Profesa Safari.

  Dk Sengondo Mvungi, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alisema Rais Kikwete ana nafasi ya kiutendaji kuhakikisha anapambana na watu wanaotuhumiwa na wanaojihusisha na ufisadi katika serikali yake.

  "Kusema Takukuru na ofisi ya DPP ndiyo inapaswa kuwashughulikia watu hao kwa kuwapeleka mahakamani ni sawa, lakini, rais naye ana nafasi yake katika hilo. Anaweza kufanya hivyo kwa mamlaka aliyonayo kama mkuu wa nchi au mwenyekiti wa chama," alisema Dk Mvungi.

  Alisisitiza kwamba, Rais Kikwete anapaswa kuwajibika kwa kuwa ndiye mkuu wa serikali inayoingia mikataba hivyo kusema kwamba hana uwezo sio sahihi.

  “Waziri Chikawe asizungumze mambo ki-uanasesere. Kwa kuwa kila hatua inayochukuliwa ikiwemo kusaini mikataba ni lazima kwanza Cabinet (Baraza la Mawaziri) ipitishe na hiyo mikataba ndiyo iliyozaa vitendo vingi vya ufisadi sasa ukisema rais hana uwezo maana yake nini? Hizo ni porojo zisizokuwa na msingi wowote," alisema Dk Mvungi.


  Dk Mvungi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR Mageuzi, alisema kutokana na mgawanyo wa madaraka katika dola Rais Kikwete anahusishwa na kila jambo linalotokea nchini kwa kuwa ndio kiongozi mkuu.


  Juzi waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe alisema Rais Kikwete hana uwezo kutumia mamlaka yake kuwapeleka mahakamani watuhumiwa wa ufisadi kwani hilo ni jukumu la vyombo alivyoviteua kuchunguza na kuchambua nani afikishwe huko baada ya kujiridhisha kwa ushahidi.

  "Huu ni utawala wa sheria, Rais Kikwete hawezi kutoa amri za kukamata watu wakati kuna vyombo alivyoviteua kuchunguza na kuchukua hatua." Waziri Chikawe alisema hayo juzi alipokuwa katika mahojiano maalumu na gazeti hili ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

  Alisema kitendo cha baadhi ya Watanzania kumshinikiza Rais Kikwete awafikishe mahakamani watuhumiwa wa ufisadi kinaashiria kuwa wanataka aamuru watuhumiwa hao wapelekwe mahakamani bila kutumia vyombo husika jambo ambalo haliwezekani katika mfumo wa kibepari.

  "Enzi zile za mfumo wa ujamaa na chama kimoja cha siasa, hilo lingewezekana, lakini wakati huu ambao nchi inatumia mfumo wa kibepari, haiwezekani," alisema Chikawe. Hivi karibuni, wanasiasa na hata baadhi ya viongozi waliowahi kuwa serikalini awamu zilizopita, wakichangia mada ya mustakabali wa taifa kwenye kongamano la Taasisi ya Mwalimu Nyerere, waliitaka CCM imtose Rais Kikwete asigombee tena ili kumalizia ngwe ya miaka mingine mitano, iwapo tashindwa kufanya maamuzi magumu ya kuwachukulia hatua watuhumiwa wa ufisadi.

  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=16685
   
 2. B

  Bobby JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Geza pole sana. I used to think it was just me who has reached this stage/level. What you have put here its like you were reading my mind. Ni aibu ni abu, I feel so sorry that this is happening in my generation and I can't help. Because the bosses (local wananchi) who pay the price of these nonsenses are completely unaware of the power they have to stop this ridiculous leadership. Mimi sijuwi kwa kweli maana unaposikia watu wanataka kuandamana kumpongeza rais kwa kazi nzuri kichwa kinataka kunipasuka kabisa kwamba tuko nao nchini wanaona yanayoendelea au wako USA?
   
 3. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,067
  Likes Received: 3,998
  Trophy Points: 280
  Meanwhile sitashangaa kama watu watanyimwa kibali cha kuandamna kama at all itatokea good will ambassador wakataka ku-riot pia ku-denounce the government!
   
Loading...