Diamond Platnumz: Kunengua kunanogesha mziki

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,982
11,393
Mwanamziki maarufu wa Tanzania Diamondplatinamuz aka chibu amerudi kutoka safari ya mbali ambapo alipiga show za kufa mtu. wakati akiwa uwanja wa ndege alihojiwa na waandishi wa habari ni kitu gani kajifunza huko kasema Kunengua jukwaani kunanogesha na kukuza mziki.

Kaeleza kule ulaya anapiga show kwa kiswahili wakati anaowaimbia wala hawajui hicho kiswahili hivyo hufurahia unenguaji na mikito midundo ya muziki na sio maneno unayoimba. hii ilinikumbusha wacongoman akina awilo madillu papa wemba walikuwa wakiimba kilingala na muda mwingine wakiimba matusi ila kwa kuwa tulifurahia unenguaji wao basi ilikuwa poa tu.

Sasa wadau wa muziki watizame namna gani watakuza tasnia ya unenguaji hasa madansa na kuimarisha mikito na midundo ya muziki. sio mtu anapanda jukwaani anaimba kama teja.
 
Kuna wale wanaojisifia wana sauti nzuri na mashairi mazuri kazi kwao,kwa mtu asiyeelewa unaimba nini sauti na mashairi yako mazuri yanasaidia nini ...lakini si mbaya kama umeamua kuwa wa hapa hapa.
 
Back
Top Bottom