Diamond katoboa pua?

kedrick

JF-Expert Member
Apr 25, 2015
5,069
4,895
Kwa niaba ya wanaume wenzangu wa Dar, naandika kwa huzuni na masononeko hii habari yako kaka Nasibu. Nikiwa ni moja wa shabiki zako toka enzi zile za Kamwambie, nimekuwa si mtu wa kuingia wala kuzugumzia personal life yako ila kama hili umenikwaza na sijui umewaza nini kutoboa pua?

Ebu sema sio kweli umebandika tu hiyo hereni, jamii inakuangalia kama fundisho kwa jinsi ulivyo hustle toka maisha magumu hadi ulipo now.

Unaifundisha nini? Nani aliokupa ushauri utoboe pua Zari, Rommy Jones au Babu Tale au yule dogo wa Empire? Mama yako je amekuruhusu?

Hayo mambo waachie wazungu wakina Chris Brown, Nasibu sio kila kitu cha kuiga bhana.

bb22583f944afda932d459bccbed4840.jpg

===========

UPDATE:

Kwa saa kadhaa zimeenea taarifa za mwimbaji staa wa bongofleva Diamond Platnumz kuonekana katoboa pua, hii habari imepewa nguvu kutokana na picha aliyoipost Diamond mwenyewe kwenye Instagram akionekana katoboa pua.

Ukweli ukoje? …ukweli ni kwamba Diamond hajatoboa pua kama wengi walivyodhani ambapo Meneja wake aitwae Sallam aliwajibu hivi mashabiki walioanza kuuliza >>> ‘Usiamini kila unachoona kwenye picha au unachoambiwa, mlikuwa mmelala sana amewaamsha kidogo’

SK.jpg


Maneno ya Meneja Sallam yanamaanisha kwamba sio kweli Diamond katoboa pua, ni mchezo tu na baada ya hiyo picha ya kutoboa pua Diamond aliweka picha nyingine inayoonekana hapa chini akiwa fresh kabisa watu wasiendelee kupanic.

Diamond-2.jpg


Chanzo: MillardAyo.com
 
hiv chimbuko la wanaume wa dar limeanzia waki kila sehemu ni mambo ya wanaume wa dar
 
Kwa niaba ya wanaume wenzangu wa Dar naandika kwa uzuni na mashononeko hii habari yko kaka nasibu nikiwa n moja wa shabiki zko toka enzi zile za kamwambie nimekuwa c mtu wa kuingia wala kuzugumzia personal life yko ila km hili umenikwaza na sijui umewaza nn kutoboa pua embu sema sio kweli umebandika tu iyo herani jamii inakuangalia km fundisho kwa jinsi ulivyo hustle toka maisha magumu hadi ulipo now unaifundisha nn nani aliokupa ushauri utoboe pua zari, rommy jones au babu tale au yule dogo wa empire na mama yko je amekurusu.? hayo mambo waachie wazungu wakina chris brown nasibu sio kila kitu cha kuiga bhn
bb22583f944afda932d459bccbed4840.jpg
uzuni =huzuni

mashononeko= masononeko

herani=hereni

amekurusu= amekuruhusu.
 
Nahisi sio kweli ngoja nipite mitaani nitarudi nikiwa na jibu maana nchi hii ukiuliza waziri wa viwanda ni nani hakuna anaemjua ila mademu wa Diamond na Kiba wanajulikana mpaka pichu zao,lazima mtaa utanipa jibu narudia tena nitarudi hapa.
 
Vijana siku hizi akisifiwa,anaanza kusuka nywele,kutoboa masikio hii nimeiona hata wachezaji wa kiafrika wanaocheza ligi kubwa za Ulaya!!
Kama ni kweli,hii itakuwa ni suala la maadili kuporomoka!
 
Unajua Mara nyingi nilikua napatashida kuhusu wasanii kua ni kio cha jamii.nimekubali kwmba jamii inaiga wasanii so kwa wasanii wetu hawa tuctegee jamii yenye maadili kila skendo mbaya ndo zao wachache wpo wanajitambua na ule msemo ya msanii ni kio cha jamii ilivyo sasa msanii ni mchafuz wa jamii wala hatuelekei kubaya tumeshafka na nishda kulud kwenye maisha yenye maadili
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom