mnyaki dada
Senior Member
- Sep 6, 2014
- 105
- 61
Kipindi ray c anakuja kwa kasi walianza kumponda sana komando...mara mbaya mara hajui kukata mara vile...matokeo yake wamebaki na aibu komando bado yupo palepale
Duh!!! Yani Mimi nimwonee wivu naseeb... Kwa umalaya,dharau,kujicfu,mpenda skendo au kwa lipi?? Me nadhani wanaomshabikia wamesharogwa vbaya sana... MTU ambaye anajiskia sip siri ananipa hasira... Eti mbeya hakuna hotel ya kulala?? Na kwao kigoma zipo?? Zaid ya lake Tanganyika?? Amesahau alivyokua anauza vocha?? Ata hizo hotelhakuwahi waza kuwa atakuja lala?? Kamweee ucsahau ulipotoka jamani... Leo yeye ndo wakumsaidi as Alikibar eti kwa kuomba korabo?!... Kama Alikibar amendharau hivo sijui wewe unajifanya shabiki anakuchukuliaje,! I think anakuchukulia kama vile ndala za kuendea chooni!! To hell na huyo Diamond wenu....!!! Guys I think we have to THINK BIG.. kama vipi mind your own issues,mana kama kazomewa tayari tushapata jibu.. Poleni kwa nyie mafuasi wake... Ila msije mkaiga mambo nimemaliza... Ucnijibu cjaulza swali hapo...ukijbu basi kimekutachi sana!! Usije na kihele hele chako kama ndugu wa mume....
tenaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Ni hivo yani ndugu yangu..... Nilivomzalendo wa mkoani kwetu Mimi afu MTU kama Naseeb akapatukanee!.... Aendeleeeee tu kumwiga Michael Jackson...
mimi nadhani Diamond kwa sasa ndio msaani anaye vizuri zaidi hapa bongo. Ushauri bora kabisa kwake kwa sasa ni kuanza kuwekeza awe na miradi ambayo itaweza kumuingizia pesa hata kama atakuwa ameshuka kimziki kuna wasanii wengi wa ndani na nje ya nchi walikuwa wanafanya vizuri kipindi cha nyuma ila sasa ni kawaida sana wale waliokumbuka kuwekeza sasa hivi wanakula kuku kwa mrija wale waliojisahau sasa hivi ni walinzi
Ni hivo yani ndugu yangu..... Nilivomzalendo wa mkoani kwetu Mimi afu MTU kama Naseeb akapatukanee!.... Aendeleeeee tu kumwiga Michael Jackson...
matumbo katika wadau wa jf ambao wako juu kwa amsha amsha, wewe ni nambari wani yaani ayena ayena. Sasa nikuulize swali moja tu, hivi kuna msanii hapa Tanzania ambaye amewahi au anaenda nchi za nje mara kwa mara kufanya show bila unga wa ... kupakiwa katika safari zake za huko nje ya Tanzania.
Duh!!! Yani Mimi nimwonee wivu naseeb... Kwa umalaya,dharau,kujicfu,mpenda skendo au kwa lipi?? Me nadhani wanaomshabikia wamesharogwa vbaya sana... MTU ambaye anajiskia sip siri ananipa hasira... Eti mbeya hakuna hotel ya kulala?? Na kwao kigoma zipo?? Zaid ya lake Tanganyika?? Amesahau alivyokua anauza vocha?? Ata hizo hotelhakuwahi waza kuwa atakuja lala?? Kamweee ucsahau ulipotoka jamani... Leo yeye ndo wakumsaidi as Alikibar eti kwa kuomba korabo?!... Kama Alikibar amendharau hivo sijui wewe unajifanya shabiki anakuchukuliaje,! I think anakuchukulia kama vile ndala za kuendea chooni!! To hell na huyo Diamond wenu....!!! Guys I think we have to THINK BIG.. kama vipi mind your own issues,mana kama kazomewa tayari tushapata jibu.. Poleni kwa nyie mafuasi wake... Ila msije mkaiga mambo nimemaliza... Ucnijibu cjaulza swali hapo...ukijbu basi kimekutachi sana!! Usije na kihele hele chako kama ndugu wa mume....
Kumekuwa na kelele nyingi sana kuhusu Diamond haswa kipindi hiki akionyesha mafanikio makubwa kimuziki.
Wakati yeye akipambana kupiga hatua kuna wanaopambana kuakikisha hasogei na anarudi chini.
Mimi nimejitolea kumpa ushauri wa bureeee kabisa akiwa kama mdogo wangu.
Ukiangalia kelele zote na matukio ya hivi karibuni utagundua hakuna ishu ya maana sana ya kumchukia diamond ila ni roho mbaya zetu waswahili...Diamond kafanikiwa sana kuna watu linawauma ili jambo yani inawauma inawauma ata wangepata nafasi ya kumuwekea sumu wangemlisha ..Jamani hakuna mtu mbaya dunia hii kama mswahili ndio maana mimi uwa sipendi kuwa karibu na mtu mswahilimswahili,nchi haiendelei sababu ya roho mbaya za kiswahili.
Mswahili anaweza kukuchukia ata hakikosa sababu ya kukuchukia na yote hii sababu ya roho mbaya unakuta mtu ana roho mbaya mpaka akicheka kuna taswira inatokea kama analia vile.
Tukifanya leo tafiti lazima tutakuta asilimia 98 ya waswahili either ni wachawi au wana tabia zote za kichawi.mbongo yupo tayari kuchoma nauli hapa mpaka nachingwea ili akakuroge kisa umenunua gari mpya, ukimpa challenge anunue la kwake atakwambia ye hapendi makuu ila atakuchukia wewe ulieamua kupenda vya kwako
Mbongo atakuchukia ata kwa kumzidi kuvaa vizuri, awezi kujipanga nae atoke smart kukuzidi ila atataka muwe wote wachafu... We ukitaka kumpima mswahili imani mkute anakula alafu akukaribishe msosi na wewe ukaribie utaona uso unavyombadilika na roho yake mbaya.
Mtu anaibuka uko alipoibuka anakwambia dogo ana dharau siku hizi, lakini ukitafakari vizuri hapa tafsiri ya neno dharau ni mafanikio....yaani tatizo dogo ana mafanikio siku hizi.
Wabongo tuna roho za kwa nini ndio maana hatuendelei kamwe, sijui tulitoa wapi hizi roho ama ni ule ujamaa ulituaribu au vipi ! ila kama ni ujamaa wenzetu China mbona wanatumia ujamaa kumfanyia roho mbaya mtu anayerudisha nyuma maendeleo ndio maana ukilisha watu drugs wanakunyonga.....sisi wabongo ujamaa wetu tunatumia kuwafanyia roho mbaya wanaopiga hatua mbele. Yani kwetu mtu akipiga hatua anafanya makosa.
So dogo diamond mimi nakushauri utulie ufanye mambo yako kimpango wako wavumilie tu awa waswahili, ila ishi nao kiakili sana. Jiamini fanya kazi nzuri zaidi watachoka tu na watakubali matokeo.
Watu wanatengeneza maneno kisha wanayapenyeza kwenye media ili kukuharibia, leo mtu anakuja na maneno eti umedharau hotel za mbeya ukimuuliza hizi kauli ulizitoa wapi hana cha kusema, kama umelala hotel za Kigoma utadharau vipi hotel za Mbeya? majuzi hapa umepiga show Tunduma inamaana huko sio Mbeya?
Unakuta mpaka radio zinaingia kwenye ujinga huu unamuuliza mtu swali akitoa majibu, mnayarusha majibu bila swali kisha mnasema haya maneno Diamond kayasema kwa Kiba. Yote ni kufitinisha tu.
Imefikia kipindi watu wanachukia mpaka wanazomea, lakini sio ishu mtu ashushwi kwa kuzomewa ingekuwa ni hivyo Chege na Temba wangeshapotea zamani maana walishapigwa mpaka makopo stejini enzi za Wanaume family na Halisi..Leo halisi wako wapi? Ata AY anayeheshimika sana kwa sasa ameshazomewa na kupigwa makopo enzi za East coast vs Temeke.
Pia chukua tahadhari na Kiba, Kiba wa sasa anamtumia diamond kupata kurudi kimuziki kiukweli bila Diamond hakuna Kiba kwa sasa but kuna Diamond bila Kiba...Kiba kwa sasa hawezi kusimama kwa kazi zake ila kwa jina la Diamond tu.
Tangu Kiba arudi kazi yake ni kuzunguka kwenye media kueleza ubaya wa Diamond, media zote kuanzia radio mpaka Tv amezimaliza akionyesha wewe ni mbaya.
Mimi nakushauri achana na kiba wewe concentrate na muziki wako kwanza mfanye kama haexist vile.
Hakuna ataekuwa juu milele ila hatushushani kwa style ya kampeni, nature ndio uwa inaamua. Muda wa mtu ukiisha haitaitajika nguvu yoyote hatutaanza kumuona kwenye headlines, hatutaskia nyimbo nzuri n.k nature itaamua.
Siku zote ridhki anayegawa ni Mungu tu hakuna binadamu anayeweza kunyang'anya ridhki ya mtu. Mungu ndio anajua nani ampe nini ndio maana yule anapewa sauti nzuri wewe ukapewa nyota. nyota ikiwaka sio rahisi kuizima ndio maana yote yaliyotokea watu wanazungumzia Diamond tu sio nani kafunika wala nini habari bado ni wewe .
Zidane alikuwa bonge la mchezaji lakini matangazo mengi na project za hela alizibeba Beckam ndio ridhki iyo kila mtu na yake.
Nakushauri fanya kazi kwa juhudi zote wataelewa tu, tena kwa sasa ndio uzidishe mara mia hasikuvunje mtu moyo bongo fleva bado inakuhitaji mno. na mashabiki wako wamezidi kukupenda amini usiamini.
Kuna wataokupenda ukifa kama Kanumba na Amina chifupa
Very true. Diamond anapashwa aajiri afisa habari wake ambaye ata deal na media. Yeye ajikite kwenye kazi ya muziki tu. Washabiki wake walimpenda sana kwa sababu wengi wao ni watu masikini sana. Hivo kwao ilikuwa ni ushindi kuona mwenzao katoboa kifani na kimaisha pia. Sasa kosa lake kubwa ni kuwadharau watu ambao ki ukweli ndo mashabiki waliompandisha huko juu.
Kuna Fiesta ya 2014 nadhani Mwanza wakati anampandisha Linnah jukwaani. Alisema ni msaani anayependa kuupeleka muziki wetu nje ya mipaka ya nchi. Na ndo maana akawa tayari kummsaidia katika wimbo wake wa Kizai zai. Maneno hayo ameyarudia kwenye interview yake na XXL kuhusu kufanya collable na Ali Kiba. Kwamba yupo tayari kumsaidia. Nadhani dogo amelewa mafanikio mapema kabla hajafika peak.
Ajifunze kwa watu kama makocha wa timu kubwa zenye mafanikio makubwa. Wakiwa kwenye interview kamwe hawawezi kuidharau timu pinzani hata kama ukweli kuwa wao wapo juu. Kocha atasema tu, namheshimu huyu kocha mwenzangu najua ana timu nzuri sana na watatupa upinzani mkali nk. Hata kama moyoni anaamini wataenda kuifunga hiyo timu. Thats the spirit.
MWISHO: Waswahili wana misemo yao ambayo tumeirithi toka kwa babu zetu mfano aliye juu mgoje chini, mpanda ngazi hushuka.Maana yake ni kuwa waswahili hatupendi kuona mtu aliyee juu anadharau maskini ambaye hana kitu. Hivyo ikibidi watakushusha kwa njia yeyote iwayo ili watumie misemo yai hii. Watch out Diamond...
Tujuze wewe kwanza... wewe binafsi au familia yako, Diamomd amewafanyia nini? Kwamba eti Masanja mbona hachukiwi sio hoja ya msingi.hujajibu swali, masanja anayo hela zaidi yao mbona hachukiwi????????/ na kipindi diamond alikuwa anashangaliwa alikuwa na maisha mabovu?
Uswahili hauwezi ishaaaa,watu wanaongeaa weeeee utadhani wanalipwa mshahara,Tanzania bila Uswahili haiendiii wengine wanajiita wasomi lakini waswahili, wanafiki,wachawiii,lakini mwisho wa siku wataongeaaa weee na watalalaaa
Wivu unatusumbua wabongo sanaaa yaan hata kwa kitu kidogo mtu anaumiaaa ndio ilivyo kwa Diamond, Ally kiba kapata kiki baada ya bifu na diamond na hiyo kuzomewaaa mbona kina Fetty waliandaa mazingira muda ule wanamsifia kiba na kusema team kiba mpooooo huo ni uchonganishiiii ,kiba alikuwepo toka zamanii kuzubaa kwake ndio kumemfanya hivyooo,Akichangamka atafika alipofika Diamond kama kuitwa kushindania tuzo, Diamond hawez kukata tamaaa,mi ningemshaurii asihudhurie hayo mafiesta yao kabisaaa afanye kama Lady jide alivyofanya basiii
(Nimeandika navyojisikia staki kubishana na mtu,toa maoni yako bila kubishana na kila mtu aandike anachojisikiaaa sio)
Hahahaa haaaa
Eti mbeya anaenda lini!