Diamond akanusha kuhusu DNA ya Tiffah

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,599
9,529
Mkali wa muziki wa Bongo fleva hapa nchini, Nasib Abdul aka Diamond Platnumz, amekanusha tetesi zakwenda kumpima mtoto wake Latiffah 'Tiffah' vinasaba 'DNA' ili kupata uthibitisho wa kuwa ni mwanawe au sio mwanae.

Diamond amezungumza hayo baada ya kufanyiwa mahojiano na eNewz kuhusiana na tetesi hizo ambapo alikanusha suala hilo, Diamond Anasema kumpima mtoto wako DNA ni kutojiamini na yeye hawezi kufanya hivyo, Diamond anasema alianza kumjua Tiffah akiwa tumboni.

Pia Diamond ameweka wazi kuwa picha inayomuonyesha akilia ni ya show yake ya Dar Live.
 
Akiamua kujibu kila tetesi atasahau kutunga mistari aharibu kazi, kukaa kimya ni jibu zuri zaidi kwake maana yanasemwa na yatasemwa mengi ukiwa star.
 
Kama yeye ni mwanaume na anajiamini akampime ajitue mzigo wa misumari..
 
yaani mondi anakua kama hajakulia uswazi, uswahilini majungu ndo kazi zetu
 
Wamuache jamaniii kila siku Mond bin Award kwani tatizo nini?
 
Back
Top Bottom