Mwanamuziki nguli wa miondoko ya Afro pop ukanda wa afrika mashariki Nasib Abdul Juma ama "Diamond" amewafurahisha mashabiki wa muziki mzuri baada ya kutangaza kuachia ngoma yake katika media za tz zote hapo kesho kuanzia saa nne huku vituo vya kimataifa vikipata nafasi ya kuuonyesha exclusive kuanzia leo hii ...
Wimbo huo utakuwa ukiitwa "nitampata wapi" ' wafuatiaji wa maswala ya Burudani wameshangazwa na Dimond kuamua kutoa ngoma kwa haraka wakati mdogomdogo ikiwa bado ipo kwenye nafasi za juu katika chati na kumbi za starehe mjini hata hivyo inatabiriwa Diamond atajivunjia rekodi yake ya kutwa tuzo saba aliyoiweka mnamo mwaka 2014 kutokana na mafanikio makubwa zaidi aliyoyapata ambayo hayajawahi kufikiaa na msanii yeyote katika historia ya muziki wa Bongofleva.
Video ya wimbo wa Diamond (ntampata wapi) ishakamilika na kabla haijaanza kuoneshwa rasmi katika vituo vya nyumbani,tayari vituo vya nje vimeanza kuionyesha na kuitambilisha, jana ilichezwa Trace tv na leo imetambulishwa kwenye kituo cha mtv base,lakini pia imechezwa kwenye tv za Nigeria ikiwemo sound city tv.
Ni utaratibu wa Diamond kuachia video na audio kwa pamoja ,ambapo kesho ndio vitaachiwa rasmi hapa nyumbani...
kwa wasiofahamu nyimbo ya ntampata wapi ni moja ya nyimbo kibao za Diamond anazorekodi kila siku aingiapo studio na nyimbo hii alianza kuitease instagram miez michache iliyopita.
sio mbaya tunavsubiri kwa hamu,ila mkuu hii mada tayari ipo ndani ya ile special thread ya diamond fans' ingekua vyema kama ungekuja kutupa updates kule ndani.
Mashairi ya wimbo ' Nitampata wapi?'
[h=2][/h]
Sura yake mtaratibu, mwenye macho ya aibu. Msahau majaribu ila namkumbuka sanaa
Umbo lake mahabibu, kwenye maradhi alinitibu, siri yangu kaharibu. Bado namkumbuka sanaa
Alienifanya silali jua kali nimtafute tukale, lakini hata hakujali mentali akatekwa na wale....X2
Kiitikio...
Nitampata wapi kama yule nampendaga sana X2
Nitampata wapi kama yule ananipendaga sana x2
Beti 2
ai nyota, nyota ndio tatizo langux2, ai nyota mpaka nalia peke yangu
ai nyota, nyota ndio shida yangu.X2
Nyota wamenizidi wenzangu,
alidanganywa na wale,wenye pesa nyumba gari, mi kapuku hakujali akanikimbia x2
alonifanya silali jua kali nimtafute tukale lakini wala hakujali mentali akatekwa na wale.
Kiitikio
Bado ananijia ndotoni,ila nikiamka simwoni.x2
Bado ananijia nikilala, haki ya Mungu sio masihara. X2
Hii ni sauti ya Rais iliyomshindaga ibilisi, kwa mwanadamu sio rais,.
Na umwambie
lazima ujue kutofautisha kati ya jumlisha na msalaba, x na zidisha.x2
Bado namuota nikilala haki ya Mungu sio masihara
Video ya wimbo wa Diamond (ntampata wapi) ishakamilika na kabla haijaanza kuoneshwa rasmi katika vituo vya nyumbani,tayari vituo vya nje vimeanza kuionyesha na kuitambilisha, jana ilichezwa Trace tv na leo imetambulishwa kwenye kituo cha mtv base,lakini pia imechezwa kwenye tv za Nigeria ikiwemo sound city tv.
Ni utaratibu wa Diamond kuachia video na audio kwa pamoja ,ambapo kesho ndio vitaachiwa rasmi hapa nyumbani...
kwa wasiofahamu nyimbo ya ntampata wapi ni moja ya nyimbo kibao za Diamond anazorekodi kila siku aingiapo studio na nyimbo hii alianza kuitease instagram miez michache iliyopita.
Na wao watakapoamua kumuyeyushia asithubutu kutuletea kelele za akina lady jay dee, mara ooh nyimbo zangu hazichezwi kwenye media za nyumbani... kwani kaamua kuwadharau na kuona sio wa muhimu tena wakati ndio waliompandisha chati.