Diamond aachia wimbo mpya "Acha nikae kimya"

Zawadi B Lupelo

JF-Expert Member
Jul 19, 2015
2,549
3,722

Ni katika wimbo wake mpya uitwao bora nikae kimya. Diamond amegusia ugomvi wa Makonda na Gwajima na ushiriki wa Mange. Amegusia tatizo la vyeti la Makonda na shinikizo la kutaka atenguliwe.​

Katika wimbo huo mpya amegusia wimbo wa Ney na kukamatwa kwa Ney, kupotea kwa Roma.

Ametumia fasihi ya hali ya juu lakini wimbo huu unamuweka kwenye kundi la waoga wanaohofia maisha yao. Diamond anasema kwenye wimbo huo ameonywa na mama yake juu ya kusema chochote kwa yanayotokea.

Anasema kumekuwa na shinikizo kutoka kwa mashabiki wakimtaka aseme chochote kuhusiana na yanayoendelea na wengine wakimtuhumu kuwa anaogopa kusema kwa kuwa Makonda ni mlezi wa Wasafi.

Diamond anasema alishindwa kupost wimbo wa nay japo ni rafiki yake wa karibu (kwa sababu ya maudhui) lakini aliumia sana Nay alipokamatwa.

Amegusia pia mgogoro ya CCM na CHADEMA.

Ametumia ufundi wa kisanaa hasa kuwasilisha ujumbe wake, lakini wimbo huu unaweza kutafsiriwa kuwa anaonyesha woga katika kuipigania jamii yake na kukemea maovu katika jamii.

Pia udhaifu mwingine ni kwamba kutumia neno "eti" kwenye swala la kuvamiwa kwa clouds media kunamuweka upande wa wavamizi kwani anatilia shaka swala ambalo ni dhahiri lilitokea
 
Huu wimbo unamuweka upande hasi kabisa asubiri criticism, he will be condemned. Siku akitekwa yeye mama yake ndiye atakayelia mwenyewe maana na wengine watakaa kimya, lakini ameimba vizuri upande wa sauti vina na muziki
 
Wewe ndio unasema juu ya uoga.

Mjifunze kuheshimu maamuzi ya binadamu wengine, sio lazima kila mtu atafute pesa kupitia kiki ya Kiongozi kwa kufata mkumbo wa uongo unaotungwa.

Mnapenda kuamulia watu kama vile, nyie mnaishi kwa kuamuliwa.

Amewapa ukweli na maisha ni yake.

Makonda oyeeeeee
 
Ninaheshimu maoni yake na mimi natoa maoni yangu jinsi nilivyousikiliza na kuuelewa wimbo wake
 
Unataka aimbe wimbo wenu wa kipuuzi Makonda amwachie Roma wakati hajamwona akimteka? tujifunze kuwa tunahifadhi maneno.
 
Jina la huo wimbo tu Mama kaniambia nikae kimya unabeba ujumbe mzito sana ambayo inaonyesha hofu iliyotanda nchi nzima sasa kufuatia vitisho mbali mbali kwa Watanzania kutoka kwenye utawala huu.

Kumbuka hata kujadili uwepo wa njaa kulitolewa vitisho mtu anaweza kuishia lupango. Yule Butiku alitoa kauli kwamba Rais anayejiona yeye ni Tembo hatufai Watanzania na kinana naye juzi kazungumza katika mistari inayoshabihiana sana na kauli ya Butiku.

Kuna wingu zito nchini ambalo limeondoa furaha na amani ya Watanzania walio wengi nchini.

Ninaheshimu maoni yake na mimi natoa maoni yangu jinsi nilivyousikiliza na kuuelewa wimbo wake
 
Diamond ni mnafiki.,ask me why,nitajibu kwa kifupi

1.kama mama yake amemwambia akae kimya kwanini katunga wimbo??Huo ndio ukimya??

Nyerere ambaye ndiye aliwekwa kwa cover ya Huo wimbo alikuwa hakai kimya,alikuwa anaonya,kukemea na Tena akawaencourage vijana wawe na ujasiri WA kuhoji,,Leo hii diamond anasema tukae kimya.,,ubashite huu.

Pia,ameonesha kukerwa na swala la kudiscuss vyeti vya bashite!!,hivyo hakupenda wimbo WA naytruboy!!!,hivyo alitaka wasanii wote wakae kimya!!!!wasihoji,,huyu kijana anawaangusha watz,,sisi tunahoji alipo Roma,wasanii wenzake wamekusanyika kutia juhudi ili mwenzao apatikane,yeye itakuwa alikuwa anarecord(hakutokea pale)

Mh,ndio sababu nilitilia Shaka ile post ya meneja wake babutale,nahisi ule ulikuwa ni mpango uliosukwa tayari,na wimbo ulikuwa tayari prepared kwa hili tukio.Hebu tujiulize,,babutale ni wa kumvimbia makonda kiasi kile kweli ???si marafiki sana na bashite???na juzi bashite alikuwa studios zao jamani???hamuoni kuwa makonda alikuwa studios kukamilisha hii project.

Na kama tale anakataa uoga(post yake insta)angemkataza diamond asirelease wimbo unawataka watu wakae kimya!cha ajabu tayari link iko kne bio yake.!!!!ajabu hii!!!!!

Kwahiyo tiffa akipotelea pasipofahamika napo atakaa kimya?au ni kwa sababu hayajamkuta yeye,??

Diamond anaplay kama snitch!na atafaidika sana kifedha na role anayoplay!!!.serikali inawapenda watu kama diamond sana
 
Wewe ndio unasema juu ya uoga.

Mjifunze kuheshimu maamuzi ya binadamu wengine, sio lazima kila mtu atafute pesa kupitia kiki ya Kiongozi kwa kufata mkumbo wa uongo unaotungwa.

Mnapenda kuamulia watu kama vile, nyie mnaishi kwa kuamuliwa.

Amewapa ukweli na maisha ni yake.

Makonda oyeeeeee
Hapo penyew teyar katafuta kiki, au haujaelewa? Kaamua kuwa tofaut na wanaopingana na serikali, kwabkuongelea matukio yaleyale bt yeye anaamin vingine, angekuwa sio mtafuta kiki angeimba kitu kinginee kabisa kisichohusiana na hali ya sasa,
 
Ni katika wimbo wake mpya uitwao bora nikae kimya. Diamond amegusia ugomvi wa Makonda na Gwajima na ushiriki wa Mange. Amegusia tatizo la vyeti la Makonda na shinikizo la kutaka atenguliwe.
Katika wimbo huo mpya amegusia wimbo wa Ney na kukamatwa kwa Ney, kupotea kwa Roma.

Ametumia fasihi ya hali ya juu lakini wimbo huu unamuweka kwenye kundi la waoga wanaohofia maisha yao. Diamond anasema kwenye wimbo huo ameonywa na mama yake juu ya kusema chochote kwa yanayotokea.

Anasema kumekuwa na shinikizo kutoka kwa mashabiki wakimtaka aseme chochote kuhusiana na yanayoendelea na wengine wakimtuhumu kuwa anaogopa kusema kwa kuwa Makonda ni mlezi wa Wasafi.

Diamond anasema alishindwa kupost wimbo wa nay japo ni rafiki yake wa karibu (kwa sababu ya maudhui) lakini aliumia sana Nay alipokamatwa.

Amegusia pia mgogoro ya CCM na CHADEMA.

Ametumia ufundi wa kisanaa hasa kuwasilisha ujumbe wake, lakini wimbo huu unaweza kutafsiriwa kuwa anaonyesha woga katika kuipigania jamii yake na kukemea maovu katika jamii.

Pia udhaifu mwingine ni kwamba kutumia neno "eti" kwenye swala la kuvamiwa kwa clouds media kunamuweka upande wa wavamizi kwani anatilia shaka swala ambalo ni dhahiri lilitokea
Uchambuzi wa Wimbo...umenikumbusha mbaliii kwa mwalimu wangu wa kiswahili kwenye uchambuzi wa vitabu na mashairi..
 
Bora tu angekaa kimya kuliko kutoa huu wimbo,tayari kashaonyesha anamtetea bashite ambaye anatiliwa mashaka kutokana na ishu za kufoji vyeti,kumiliki magari ya watu aliowataja kwenye matumizi/biashara ya madawa,kuvamia clouds media,tukumbuke alimpiga Warioba........
Bora kukaa kimya kuliko kuongea pumba ukaharibu cv yako,mondi kaonyesha kuwa ni pumba
 
Nimesa comment zenu wengi naona uchambuzi wa sanaa umewapita kushoto,jaribuni kuchukua muda wenu msikilize walau mara mbili mara tatu mtamuelewa sana diamond,mama ake kamwambia akae kimya...je ukisikiliza hiyo nyimbi mmeuona huo ukimya? Kaongelea masakata ya vyeti vya bashite, kaongelea kuhusu nape,roma na bunge...mwishoni akawa anaisikitikia tanzania wapi tunakoenda....sanaa inahitaji mtu utuluze akili sana ili uielewe
 
Bora tu angekaa kimya kuliko kutoa huu wimbo,tayari kashaonyesha anamtetea bashite ambaye anatiliwa mashaka kutokana na ishu za kufoji vyeti,kumiliki magari ya watu aliowataja kwenye matumizi/biashara ya madawa,kuvamia clouds media,tukumbuke alimpiga Warioba........
Bora kukaa kimya kuliko kuongea pumba ukaharibu cv yako,mondi kaonyesha kuwa ni pumba
Ni kweli angenyamaza hakuna cha maana alichoimba ni unafiki dai naye zero hamna kitu
 
Back
Top Bottom