Di Maria ajuta kujiunga na Man United

Di Maria ajuta kujiunga na Man United

fungi

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2014
Posts
2,539
Reaction score
4,676
Mchezaji nyota ambaye pia ni kiungo wa kati wa Manchester United Angel Di Maria amesema kuwa alifanya makosa kujiunga na Kilabu ya Manchester United msimu uliopita.
Raia huyo wa Argentina amejaribu kuingiana na maisha ya ligi ya Uingereza na majuto yake yataongeza uvumi kwamba anapanga kuondoka katika kilabi hiyo miwshoni mwa msimu huu.
Mwandishi wa Uhispania Manolete Esteban anadai kwamba mchezaji huyo wa zamani wa kilabu ya Real Madrid ambaye amekosolewa kwa uchezaji wake amewaambia marafiki zake kwamba anajuta kuondoka katika kilabu ya Real Madrid.
Esteban aliiambia runinga ya Uhispania katika kipindi cha La Goleada kwamba Di maria alikiri kwa rafikiye katika kilabu ya Real Madrid kuwa anajuta kujiunga na Manchester United.
140914190818_angel_di_maria_man_united_1_512x288_reuters.jpg

source:BBC
 
Siyo kweli kasema anafurahi maisha ya Mancherster Utd.
 
kwani atakaa hapo hadi mwisho wa maisha yake mkataba ukiisha asiongeze aende mi nahis hata jez namba 7 inamtesa tofauti na hawa

7--- cantona ,, beckham ,, ronaldo saiv inamtesa di maria

9--- nimeiona akivaa andy cole toka aondoke hamna aliyotamba nayo babatov na luis saha iliwatesa + falcao now

11--- nimeiona akivaa giggs saiv inamtesa januzaj mbaya
 
Na yeye acheze mpira sasa aachane na blah blah, kama hataki arudi kwao Buenos Aire akacheze tango.
 
Nilikuwa na matarajio makubwa kwake,anacheza kwa kiwango cha chini yampasa ajitazame upya,ManU wamelipa fedha nyingi mno...babu Van Gaal Kama anazingua mpe nafasi dogo Januzay,yeye piga bei....
 
Kabla ya kuondoka Real Madrid alikuwa hivyo hivyo vijineno vya chini chini tu kila siku. Watu wanakulipa hela nyingi cheza mpira, kama hutaki ondoka kuna watu wanalilia hizo nafasi.
 
Kama Di Maria angekuws anaccheza vizuri halafu wenzie wanaharibu ningemwelewa! Lakini yeye ndio kinara wa kuharibu uwanjani! Mechi iliopita kaharibu mpaka kaingizwa do go Januzaj na dogo akabadili mchezo!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom