Dhuluma ni mbaya sana.

jf user

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2018
Posts
777
Reaction score
625
Hakuna kitu kibaya duniani kama kuchukua au kudhulumu haki ya mtu.
Kuna watu hawastahili lakini wanatumia nguvu kupata hicho wakitakacho kwa mtu kwa namna yeyote ile isiyo halali.
Matokeo huipata hiyo haki ambayo hawastahili huku kumuacha huyo mtu walimdhulumu akiwa katika ukiwa na majonzi makubwa ila kwa kuwa hana uwezo inambidi akubaliane na hali maisha yasonge.

Matokeo ya ufedhuli wote ni laana kwa watendaji/wahusika wao na vizazi vyao kama maandiko matakatifu yanavyosema.
Vitu batili havidumu kwani vina ukomo na hili hujidhihirisha kwa jamii inayozunguka watendaji.

1/Malipo ni hapa hapa dunini. Ukiisikia KARMA Ndio kwamba ufanyacho ndicho ufanyiwacho.
2/Ukiishi kwa upanga lazima ufe kwa upanga.
3/Apandacho mtu ndicho avunacho kama ulipanda panapostahili basi tegemea kuvuna kinachostahili ila kama ulipanda pasipostahili hesabia kupata kisichostahili.
4/Muda ni jibu la wote haya kwa waliodhulumiwa.
5/MUNGU huwaokoa wale watu wake wote watesekao na kuwaweka mahali salama.
6/MUNGU ni mwema kwa wote wamtegemeao, MUNGU ni wa haki kwa wote pasipo upendeleo.
 
Hio misemo ya mfa maji tu haishi kutapa tapa. Kama kweli karma inafanya kazi naona karne zinapita wazungu wanazulumu tokea Roman empire mpaka British na America hakuna karma hata moja iliowafika.


Ndukiiiii πŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈ
 

Dohhh wewe ni noma
 
Safari ya malipo haiishii hapa duniani tuu mkuu bali motoni nako karma inaendelea.
Kuhusu hizo tawala kubwa kwa kweli zina mwisho wake watu wake huishia pabaya hasa wanajeshi.
We jiulize tawala zilizoutisha ulimwengu kama babuloni, medi na aujemi, ugirikii, ottoman, na nyingine nyingi zipo wapo?
Kimsingi zimeshakufa kilichobakia ni magofu na nyingine hazijulikani kabisa.
Kila kitu hulipiwa, karma huja kwa namna mbalimbali.
Kwa mfano majuzi hukusikia mtu kauawa na mumewe? unadhani yote hayo yanatokea kwa sababu gani?
Yakupasa usome kwanza biblia ndipo umtambue MUNGU hivi hivi huwezi elewa ila wahusika wanaelewa.

Binadamu ndio ambao hufikwa na hizo karma kwani dola inajengwa na nani?
 
1/Malipo ni hapa hapa dunini. Ukiisikia KARMA Ndio kwamba ufanyacho ndicho ufanyiwacho
Nimesema hio misemo ya mfa maji haishi kutapa tapa. Sasa soma huo wako unasema malipo baada ya kufa au? Kuhusu dhulma haidumu sasa kuna binaadamu yupi ataishi milele? Dhulma ipo palepale ila mfumo wake unabadilika, ndio nikasema Roman empire, British na America hao wana historia ya kuzulumu tu na kuwafanya watu watumwa. Au ndio unasubiri kuna siku na sisi waafrika tutawazulumu na kuwafanya watumwa na wao?


Ndukiiiii πŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈ
 
Ukiona umedhulumiwa ujue na wew umedhulum sehem Acha upigwe tu km sio wew basi babu yako mza babu yako alidhulum karma imekuangukia wew
 
Mkuu huo msemo wa malipo ni hapa hapa duniani ni wa waswahili ndio maana tumezoea kuutamka pasipo kuangalia kwa kina dhambi zinavyokwenda.
Ila kwa nijuavyyo mimi dhambi hulipwa na mhusika hapa duniani au dhambi ikaenda mpaka kwa uzao wake hadi kizazi cha nne. Pamoja na yote hayo kuna kwenda motoni.
Kwa hiyo utaona kuna dhambi za duniani na huko motoni.
Yote ni matokeo ila tambua tuu MUNGU ni wa haki siku zote kila kitu hulipiwa.

NB: Ukipata ushuhuda ndipo utakubaliana na mimi, najua binadamu huwa hatuamini mpaka tuone/tushuhudie kwa macho yetu.
 
Ukiona umedhulumiwa ujue na wew umedhulum sehem Acha upigwe tu km sio wew basi babu yako mza babu yako alidhulum karma imekuangukia wew
Hongera mkuu usemalo lipo ila wengi huwa hawatambui hilo labda kwa wenye Imani ya MUNGU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…