dhulum

dhulum

Sir-mganah

Member
Joined
Jul 17, 2011
Posts
58
Reaction score
11
DHULUMA, DHULUMA, DHULUMA IRAMBA MAGHARIBI !!!!!!!!!!!! WAPI MBUNGE WANGU MWIGULU NCHEMBA…………….
Kwa kujikumbusha tu niliandika taarifa kama hii mwaka jana na Mbunge wangu Mh. Mwigulu Nchemba aliahidi kuifanyia kazi na bila shaka aliitekeleza na sasa limeanza tena.
Kama kawaida yangu napenda sana kwenda nyumbani kila ninapopata fursa na sasa niko huku Wilayani IRAMBA kata ya kinampanda kijiji cha Galangala, Munkonze. Naonana na kukutana na wazee na akina mama waliojaa nyuso za majuto, ghadhabu na vilio visivokwisha kama yatima walioachwa nyikani bila kujua ni wapi wataiona njia ya matumaini. Hii inatokana na ukatili wa kutisha unaoendelea kufanywa na askali wa migambo wanaoshirikiana na maofisa wanaijiita wa halmashauri ya wilaya ya Iramba kupita kila nyumba na kukusanya kodi za mifugo ikiwa ni shilingi elfu moja kwa kila ng’ombe na shilingi miatano kwa kila mbuzi,kondoo na nguruwe.
Watu wanaoshindwa kulipa kodi hiyo wanakamatwa na kwenda kutupwa lupango huku wengine wakinyang’anywa baadhi ya mifugo yao kwa madai kwamba ni fidia ya ushuru wanaotakiwa kulipa. Jamani jamani uko wapi utu wetu sisi watoto wa wakulima? Mateso haya hata lini? Uonevu huu mpaka lini? Alihoji bi kizee mmoja aliyejitambulisha kwa kina la Namakala.
Hata hivyo watu wengi wanahoji uhalali wa kodi hizo wakati ambapo hakuna hata chembe ya msaada wa serikali juu ya ukuzaji na uendelezaji wa mifugo yao.”dawa tunanunua kwa pesa zetu tena nyingi, sehemu za malisho tunataabika hatujaona hata ofisa mmoja wa halmashauri anakuja kutusaidia hata kuchimba kisima kimoja tu cha kumyweshea mifugo yetu kila kitu tunafanya wenyewe halafu leo wanakuja watu ati wanakusanya kodi ya mifugo inaenda wapi?” walihoji baadhi ya wazee huku wakitokwa na machozi kwa uchungu.
Naiomba serikali yangu ilifuatilie jambo hili kwa ukaribu na kwa umakini zaidi ili kuwapa ahueni ya maisha watu wa jamii hii. Nawakilisha ………………No politics
 
Back
Top Bottom