Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 122,490
- 96,054
Wana jamvi kumekuwa na dhana hii ya wachawi kula nyama za watu na hii inajitokeza sana mikoa ya Kanda ya Ziwa, kuna wakati nilikuwa nasoma Bukoba kuna mwanafunzi mwenzetu yeye ni mtu wa huko alifiwa na mdogo wake hivyo akaenda kwenye msiba na alivyorudi shuleni ktk mazungumzo yetu juu ya misiba ndio akaongelea juu ya imani ya wachawi kuwa wana uwezo wa kwenda kwenye kaburi na kumfufua maiti kumtoa kaburini bila ya kufukua kaburi,wengi tulishangaa ni wapi hao watu wanapata uwezo wa kimiujiza. Je, ni kweli kuna miujiza ya namna hiyo?
Mshana jr tafadhali karibu
Mshana jr tafadhali karibu