Dhana ya mafiga matatu kwenye ndoa

Didododi

JF-Expert Member
Jul 21, 2023
321
426
Wanajukwaa kuna hii dhana ya mafiga matatu ambayo imekuwa ikisikikasikika. Na imekuwa ikisemekana wakati mwingine inazungumziwa hata kwenye mazungumzo official kama kitchen parts ambapo mhusika huusiwa kwamba ili nyumba iwe stable haiwezekani unless yawepo mafiga matatu.

Kulingana na wadau kadhaa ambao nimefanyiana nao mahojiano wanasema msisitizo unatolewa kwa wahusika,kuwa chungu hakiwezi kuivisha pasi na mafiga matatu. Binti anapokuwa anaolewa it's said dat Maza awezampa hii siri mwanae.

MAMA: Mwanangu unaolewa lakini nina neno dogo kwako.
BINTI: Niambie mama
MAMA: Binti yangu huko uendako ishi vyema na watu, mheshimu mumeo ndugu na marafikize lakini pia kuna kitu cha msingi nataka nikugusie mwanangu!
BINTI: Nakuskiliza mama
MAMA: Mwanangu Katika harakati zako kumbuka figa moja haliivishi chakula
Binti: Unamaanisha nini mama
MAMA: Mwanangu mwanaume mmoja hakidhi
Binti: Mmmmmh mbona mama skuelewi.
Mama Mwanangu Ipo siku utakujaelewa ninachokueleza
Binti:🥱

Kama ni kweli binti aweza usiwa haya kwenye official occasion, na official personnel Hivi kweli hii haiwezi chochea kutokuwepo uaminifu kwenye ndoa.
 
Unataka kusema hadi mzazi wako wa kike ana mafiga matatu? Dada zako je? Shangazi zako nao vipi,
Hebu anza kuwauliza hao wote kisha utupe mrejesho
 
Back
Top Bottom