Saikolojia: Fahamu magonjwa ya kisaikolojia, dalili,tabia na mifano.(Case study Tanzania)

Education Mentor

JF-Expert Member
Oct 26, 2016
396
687
Saikolojia: fahamu magonjwa ya kisaikolojia common tanzania na tabia zake.

Fahamu magonjwa ya akili ambayo yapo katika jamii zetu na dalili zake.

Habari za leo msomaji wangu wa makala zinazohusu saikolojia na maisha kwanza nikiomba radhi kwa kushindwa kuiposti sehemu ya mwisho ya makala inayohusu “Furaha” kutokana na ushauri nilioupata kwa memba wengine.

Leo makala yangu ninajikita katika kuangazia baadhi ya magonjwa ya akili ambayo katika uzoefu wangu nimeyaona hapa nyumbani Tanzania kwa baadhi ya watu wenye hadhi tofauti tofauti katika mazingira ya jamii zetu.
upload_2018-4-13_15-13-46.png

(Dalili mojawapo ya ugonjwa ya akili unaoitwa histrionic personality disorder)

Kwahiyo niviweke masuala haya sawa kabla sijaanza makala;

Kwanza katika kujadili magonjwa ya akili vipo vyanzo vingi tu vinavyosabababisha magonjwa haya na vingine si rahisi kuvielezea pasipo kugusia masuala ya kiroho na imani mfano radhi ya wazazi na laana.

Lengo la somo si kuwahukumu watu, bali kubadilisha fikra na mitazamo ya wasomaji wa makala nazoandika na jamii yote kwa ujumla. kusudi wale wenye majeraha katika nafsi zao (kutokana na matendo au mahusiano ya wenye shida hizo) wapate msingi mpya kuelewa na kupona.

Na kama ni ndugu, rafiki au jamaa uangalie namna unaweza msaidia kwanza kwa busara zote sababu hapa afrika kumuambia mtu ni mgojwa wa akili ni sawa na kumtukana.

Hivyo lengo la makala hii ni kuelimisha jamii kwa nia ya kujenga.

SEHEMU YA KWANZA

Nini maana ya magonjwa ya akili au ya kisaikolojia? (Mental disorder or psychological disorder)

Katika kutafsiri dhana hii ya magonjwa ya akili ni muhimu kuanza kwa kueleza kipengele muhimu tabia zisizo za kawaida (Abnormal behavior).

Katika saikolojia “abnormality” ni pale mtu anapokuwa anafanya au anaonesha tabia ambazo si za kawaida kulingana na jamii husika.

Hivyo kwa dhana hiyo ijapokuwa nimetafsiri kwa ufupi sana hivyo magonjwa ya akili ni tabia au utendaji wa akili ambao unasababisha au unamtofautisha mtu katika namna ya matendo au utendaji, maamuzi yake hasa katika jamii yake.

Yapo katika makundi mengi ambayo ni Anxiety disorders, eating disorders, mood disorders, neuro developmental disorders, personality disorders, psychotic disorders na substance use disorders.

Lakini katika uchambuzi wangu nimeyaangazia ambayo nimeyaona katika mazingira ya jamii yetu nyumbani hivyo nimechomoa chomoa baadhi tu ambayo yapo katika jamii zetu na mifano kutokana na uzoefu (experience) na watu hao.

1. BIPOLAR DISORDER

Huu ni ugonjwa wa akili ambao nina uzoefu sana na mtu ambaye anaugua tatizo hili na nilishawahi elezea katika makala zangu kwa kifupi hasa ile “inayohusu tabia ya hasira”.
upload_2018-4-13_15-14-4.png

(Mwanafunzi huyu aliyekumbana na hasira ya walimu walio katika mafunzo kwa vitendo kutokana na maelezo niliyoyapata kutoka kwa walimu wake shuleni, hasa ripoti ya maendeleo ya tabia zake alikuwa na moja wapo ya dalili za bipolar disorder)

i. Tafsiri

Bipolar disorder hutokana na shida katika kemikali muhimu sana katika ubongo wa mwanadamu serotonin, dopamine na norepinephrine (Neurotransmitter) hivyo kunapokuwa hakuna mlinganyo sawa wa kemikali hizi ndipo hutokea matatizo haya na uathiri sana mood ya mtu huyo.

ii. Namna unavyojihidhirisha katika tabia

a) Kitabia watu wenye bipolar dis order hawatabiriki tabiriki katika mood sababu leo mnaweza mkacheka vizuri tu mkapanga hata na mipango mizuri tu. dakika hiyo kabadilika

b) mara nyingi kisirani kisirani, unyanyasaji, kiburi hivyo unathiri hadi maamuzi yake anapokuwa wakati ana hasira hayaelezeki. lakini baadae unakuta anarudi anakuwa mtu mzuri tu kama hakuwa yeye vile.

c) Pia Bipolar uathiri tabia hasa mahusiano hasa kushindwa jidhiti katika tamaa za mwili hivyo kama ni mwanaume anaweza akatembea na wafanyakazi wa ndani au kubadili wanawake mara kwa mara pia mwanamke hutokea.

d) Pia kupigana na kupiga watu ni sifa mojawapo ya bipolar dis order (Chris Brown ni muathirika wa Bipolar Disorder).

iii. Kipi kinasababisha?

Kama nilivyoeleza hapo awali shida ya mlinganyo wa kemikali Sababu za genes ni ugonjwa wa kurithi, matumizi ya madawa vibaya hospital au vilevi kukumbwa na msongo wa mawazo kwa kipindi kirefu na pia matukio ya kunyanyaswa hasa wakati wa utotoni.

2. OBSESSIVE COMPULSORY DISORDER.
upload_2018-4-13_15-14-15.png

(“..Huwa nasumbuliwa na ocd hivyo najikuta kila kitu lazima kiwe lazima kiwe katika mstari au kwa pair hata ninapokwenda hotelini kabla zijapumzika huwa ninahakikisha ninaanza kupangapanga…”David Beckham)

i. Tafsiri yake

OCD ni ugonjwa wa akili ambao husababisha mtu kushindwa jidhibiti fikra au mawazo na kuvifanya vitu kwa kujirudia mara kwa mara. Au mawazo yanakuwa yanajirudia jirudia au picha katika fikra na mtu anashindwa zidhibiti.

ii. Namna unavyojihidhirisha katika tabia

a) Mtu mwenye ocd sababu msingi wa ugonjwa huu ni aina flani ya hofu au wasi wasi kwahiyo kama ni nyumbani ndani anaweza akarudia usafi sehemu moja tu zaidi hata ya mara tano hata kama tiyari ni pasafi.

b) Kama ni usiku muda wa kulala anaweza usiku kucha akawa anatoka kwenda kuhakikisha kama mlango umefungwa vizuri wakati kafunga yeye mwenyewe.

c) Kama ni upangaji nyumbani basi kila mara yeye ni kupamba tu, Hivyo unaweza kukuta shughuli hiyo hiyo akarudia kutwa nzima ili mradi kila kitu kiwe perfect.

d) Kama ni mtihani anaweza akamaliza mapema lakini anaweza akajikuta anafuta hata majibu mazuri akaanza andika majibu ya uongo, wakati mwingine akashindwa maliza mtihani sababu ya kurudiarudia na kuhakikisha.

e) Wakati wote anajikuta katika hali kutaka kila kitu au mazingira yawe kamilifu na timilifu “Perfect”.

iii. Kipi kinasababisha?

Huu ni ugonjwa wa kurithi kwa mujibu wa tafiti pia unasababishwa na matukio wakati wa utotoni hivyo wazazi kuweni makini wakati wa malezi yenu.

3. HISTRIONIC PERSONALITY DISORDER
upload_2018-4-13_15-14-27.png

(Maisha ya “video and slay queen" mmoja hivi niliyewahi kumfahamu kwa karibu).

i. Tafsiri yake

Huu ni ugonjwa wa akili unaosababisha mtu kutafuta kuangaliwa kuonekana kusikilizwa na kila mtu hii ikiambatana pia na hata tabia ya kukaa uchi au kupiga picha za nusu uchi hasa kwa wadada (kama ni mwanaume rejea picha ya mwanzoni mwa mada). Hata wanaume uugua huu ugonjwa lakini kwa mujibu wa tafiti unaathiri sana wanawake.

Hivyo maelezo yangu nitaegemea sana kwa wanawake katika maelezo yangu

Mfano

Kuna msichana mmoja nilifahamu ana tatizo hilo kupitia kipindi hicho cha urafiki wake dada (mdogo wangu wa kike) amekuwa maarufu sana kwa picha zake mitandaoni hata kwenye magazeti hasa ya udaku kutokana na picha zake zenye utata utata mtupu na namna anavyoishi kimaigizo.

hapo zamani kabla hajawa maarufu alikuwa akija mara kwa mara kumfuata mdogo wangu. Huyu ana umbile zuri kwa macho ya waafrika. Na kutokana na hilo imekuwa kawaida sana kujipiga picha zenye utata yaani ukizitazama ni kama “pornographic” vile.

Lakini nikabidi ni mchimbe dada yangu anielezee maisha ya kwao huyu dada katika vitu baadhi alivyonieleza kuhusu mazingira ya ukuaji wake na tatizo la ulevi wa baba yake na pia kukua huku kutokuwa na ukaribu sana naye.

Hapo nikagundua tatizo lake “ni njaa ya upendo wa baba” au kutopata upendo wakati akiwa bado mdogo “Oedipus complex”, hivyo tangia siku hiyo niliacha kumuhukumu nikamuonea huruma kwa kweli nikajua kuna kitu alikiruka kikaja jitokeza kwa namna hiyo hapo baadaye.

ii. Namna unavyojihidhirisha katika tabia

a) Kuishi nje ya uhalisia maisha ya maigizo kwa sanaa,

b) anaweza kuvaa nguo ambazo si rahisi katika jamii mtu mwingine kuvaa vivazi vya utata,

c) kutakakuwa kama habari ya mjini kama sasa tungesema “kiki” kuanzia mtaani hata katika jamii.

d) huwa hana uvumilivu kabisa

e) wakati wote kuwalaumu wengine kwa kushindwa kwake.

iii. Kipi kinasababisha

a) Malezi hasa kukosa upendo au ukaribu wa wazazi wakati wa utoto hivyo njaa au kiu ya upendo hurudi kipindi cha ujana.

b) Pia ni ugonjwa pia unatokana kwa ya kurithi.

4. GAMOPHOBIA
upload_2018-4-13_15-14-41.png

(“..bado nipo nipo kwanza unasema!? Wakuoa nitakuwa mimi bwana...”)

i. Tafsiri

Hii ni hali ya kuogopa au wasiwasi katika kufanya maamuzi “Fear of commitment” mara nyingi sana inaelezewa hasa katika hofu ya kuoa au kuolewa na watu wa aina hii huwa hawana maelezo ya msingi basi ni kwanini wanafanya hivyo na wakati huo umri wao unazidi kwenda.

Pengine ushakutana na mtu awe mwanamke au mwanaume unapoanza kujadili masuala ya kuoa au kuolewa basi atakwepesha mada au atataka kuondoka kijweni hapo.

Mfano

Nakumbuka miaka hiyo bado nikiwa chuoni ilitokea darasani kukatokea mada hiyo mkufunzi (Lecturer) wetu akaanza kut hadithia kuhusu rafiki yake mmoja aliyekataa kabisa kuoa. Sababu akiwa bado mdogo lakini akijitambua kabisa mama yake alimbeba mgongoni (sababu aliona huyu mtoto ni mdogo sana kuweza pembua mambo).

Akaenda naye kwenye “masuala ya jando na unyago kuwafunda watoto wakike”. Hivyo masuala aliyoyasikia kadili alivyokuwa anakua akazidi kuyaelewa kwa kutafsiri mazingirani ya kwao ikiwemo mojawapo ya “mafiga matatu”.

Hivyo baada ya hapo kiukweli kafikia mtu mzima lakini hataki kusikia kabisa masuala ya ndoa.

ii. Namna unavyojihidhirisha katika tabia

a) Anaweza akawa tayari wakati mwingine anaishi kinyumba na mwenza na wamepata watoto lakini linapokuja suala la kujadili kuoa au kuolewa hatakwepesha mada au kuwa mkali tu.

b) Wakati mwingine anajifahamu hofu yake hiyo lakini tatizo anashindwa jidhibiti tu.

c) Sababu nyingine ni uoga wa kujitoa katika maisha na mtu mmoja tu mpaka hasa kwa kuzingatia neno mpaka kifo kiwatenganishe”.

d) Sababu nyingine zinahusiana na wasiwasi kuhusu kipato kuweza hudumia au woga usio na maelezo kuhusu “kesho yetu”.

iii. Kipi kinasababisha

(Kwa mujibu wa wanasaikolojia na uzoefu wangu katika jamii yetu)

a) Matukio wakati wa umri mdogo (Mfano binti anapoona mama yake anavyonyanyaswa na baba yake) au matukio kama aliyoyashuhudia niliyekupa mfano pia.

b) mtazamo mbaya wa fikra kuhusu ndoa na pia tatizo hili ni la kurithi na hofu ya kifedha na kubeba majukumu.

ITAENDELEA TENA KATIKA SEHEMU YA PILI USIKOSE.

Pia ili huweze kufuatilia vizuri mafundisho haya kuhusu Saikolojia na maisha ni vizuri kama utaanza ni follow katika akaunti yangu “Education mentor” pia niombe radhi tu kwa wale walioniomba kuwatag hinaniwia vigumu kukumbuka majina yote.

Na pia kuhusu Maswali yoyote ya kisaikolojia na maisha unaweza niuliza PM na mimi ntayajibu kwa mfumo wa makala au “mada” kipengele natazamia sana kukianzisha siku za usoni.

KUHUSU MWANDISHI,

Education Mentor ana shahada ya Saikolojia, ni mwanasaikolojia anayeegemea kutambua uwepo na asili ya Mwanadamu inatokana na Mungu (Creation Theory).

Pia ni Msomaji wa Vitabu vinavyohusu Falsafa, Nyurolojia, Historia, Maandiko pamoja na Vitabu vinavyooelezea maisha ya watu mashuhuri (Biography book).

Makala nyingine alizoandika Education Mentor..
Saikolojia: Fahamu tabia ya hasira, madhara yake na namna za kuishinda

Saikolojia: Sababu zinazosababisha magonjwa ya akili ambazo wengi hawafahamu. (psychological disorder)

Saikolojia:Jifunze mambo yakayokusaidia kuwa na maisha yenye furaha (Case study Finland)

Saikolojia: Jifunze mambo yatakayokusaidia kuwa na maisha yenye furaha (sehemu ya pili)
 
mimi natakaga kama nmepiga deki ndani basi pabaki hivyo hivyo,au chooni pabaki hivyo hivyo, pakivurugwa naenda kuweka sawa, hata kutwa nzima
kwahiyo na mm nna OCD
 
hyo ni dalili moja wapo kama inapozidi saaana tabia hyo hadi inakupa kero hata wewe mwenyewe
Mi hainipi kero ila atakaekuja kuvuruga nilipopanga ndo hatari inaanzia hapo,hata nisipomwambia nimekwazika ntabaki nimenuna huku namchekea,nanung'unika siku nzima yaani nahisi amedharau nilichokifanya
 
Wasomaji wangu kuna kitu nacho unaposoma dalili flani za ugonjwa Mara nyingi wengi ujihisi hivyo hata kama hawana shida yoyote
 
Mi hainipi kero ila atakaekuja kuvuruga nilipopanga ndo hatari inaanzia hapo,hata nisipomwambia nimekwazika ntabaki nimenuna huku namchekea,nanung'unika siku nzima yaani nahisi amedharau nilichokifanya
Kama hinafikia kukupa tabu wewe au watu wanaokuzunguka ni dalili hiyo inapofika hatua ya kutokuwa sawa abnormality
 
Ahsante sana Mkuu kwa mada yako iliyojaa utilio na madude ya uhakika.

Binafsi huwa ninapenda sana kufuatilia mada zako na kwa kweli huwa ninjifunza mengi sana.

Shida yangu ni moja: huwa ninakereka sana pale unaposhindwa kutofautisha wapi uweke "h" na wapi uache. Kwa mfano neno inaniwia ukiandika huwa unaandika "hinaniwia".

Je, huo nao ni ugonjwa wa Kisaikolojia au ndio OCD?
 
Ahsante sana Mkuu kwa mada yako iliyojaa utilio na madude ya uhakika.

Binafsi huwa ninapenda sana kufuatilia mada zako na kwa kweli huwa ninjifunza mengi sana.

Shida yangu ni moja: huwa ninakereka sana pale unaposhindwa kutofautisha wapi uweke "h" na wapi uache. Kwa mfano neno inaniwia ukiandika huwa unaandika "hinaniwia".

Je, huo nao ni ugonjwa wa Kisaikolojia au ndio OCD?
Shukrani mkuu....hata Mimi pia nina kasoro hiyo bado nafuatilia sijapata jibu
 
Back
Top Bottom