Mondoros
JF-Expert Member
- Aug 29, 2015
- 629
- 472
VIPIMOMO VYA UKUAJI WA UCHUMI
Kuna njia nyingi za kupima ukuaji wa uchumi ila njia kuu zipo mbili ambazo ni pato la mtu mmoja mmoja (per capita income) na pato la taifa (GDP)
1. Pato la mtu mmojammoja( per capita income)
Wachumi wengi wamekuwa wakisema kuwa njia bora ya kupima ukuaji wa uchumi ni namna kwa kuangalia pato la mtu mmoja mmoja kwa kuwa wanaamini njia hii ni jumuishi(ukuaji wa uchumi unaneemesha mtu mmojammoja). Wengi hata wale wasiowachumi(wazee wa ukame) wanataka iwe hivii,ila changamoto yah hii ni hasa kwa nchi zetu ambazo maskini ni wengi kuliko matajiri(wenye mapesa mengi mno) ni kuwa Babu Tanzania ataonekana na mapesa mengi kumbe nashindia muhugo mkavu na maembe iloa Bakresa kanigawia fedha zake kidogo ili namimi nionekana nimo nimo kwenye chati ya wenye fedha angalau. Njia hii inamfanya masikini kuwa na maisha ya kati na tajiri kuwa na maisha ya kati kwenye takwimu za kidunia wakati uhalisia haupo hivo. Tatizo linguine la hii njia inawezakuonesha uchumi wa Rwanda ni mkubwa zaid ya uchumi wa marekani kutokana na idadi ya watu baina ya hizo nchi(population size)
· Per capita income= pato la taifa (GDP)/idadi ya watu katika taifa(population size)
2. Pato la Taifa (GDP)
Pato la taifa ni jumla ya mapato yote yanayokusanywa na serikali kutoka katika vyanzo vyake vyote vya mapato pamoja na mapato ya sekta binafsi zinazofanyakazi ndani ya nchi husika kwa mwaka. Serikali nyingi makini na hupenda kuona pato la taifa linawanufaisha wote ndo maana hujikita zaid kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo na huduma za jamii kama shule,hospitali, ujenzi wa viwanda, ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji(barabara,reli,bandari,viwanja vya ndege nk) kuliko katika matumizi ya kawaida (kulipa maposho yasiyo na msingi,safari za ndani na nje zisizo na msingi,nk).
Sasa Uchumi wa Taifa unakua kwa asilimia 7.2 na nchi yetu imekuwa miongoni mwa nchi 20 duniani ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi kwa mujibu wa ripot ya benki ya dunia. Je unajua kwanini watu wanasema pesa zimekauka mifukoni??,,sababu ni moja tu watanzania wengi tumewekeza kwenye kutumia pesa kuliko kuzalisha fedha,yaan hatuwekezi kwenye miradi ya maendeleo.
JINSI YA KUPAMBANA NA UKAME WA MFUKONI
Njia pekee ya kufanya pesa ziingie mifukoni kila dakika ni kufanya shughuli za uzalishaji. Serikali ya sasa inatengeneza miundombinu salama ya watu kuzalisha na uzalishaji wao kuwa na tija, unahamasisha watu kufanya kazi hivyo basi kama utaendelea kukaa vijuweni kusubir mifuko icheke itakula kwako. Kuongeza ubunifu ndio silaa kuu zaidi maana Tanzania inafursa kila kona ila watanzania wengi hatuzichangamkii.
Mwisho.