ideal safarimate
Member
- Mar 17, 2016
- 71
- 91
Taifa letu kwa mara ya kwanza (baada ya baba wa taifa) limepata rais jasiri na mwenye dhamira ya kweli kusimamia rasimali za nchi.Ndani ya kipindi kifupi cha takribani miezi 5 amevumbua uozo uliokuwepo kwenye taasisi za serikali ambazo "wezi" waligeuza shamba la bibi.
Pamoja na mambo mengi mazuri lakini ukweli unabaki kwamba raisi Magufuli ni binadamu hivyo yapo baadhi ya mapungufu kwenye maamuzi na kauli zake kwahiyo si vibaya tukiyatanabaisha kwa lengo la kujenga.
Kauli na msimamo wa raisi kuhusu lengo lake la kushusha mishahara ya watumishi hasa kwenye taasisi na mashirika ya umma katika ngazi ya juu hasa wakurugenzi isizidi million 15.
Kwanza niweke wazi naelewa dhamira(spirit) ya raisi kuweka usawa(fairness) wa maslahi ya watumishi wa ngazi za chini na juu.Lakini tuseme ukweli kwamba usawa ni jambo muhimu lakini wakati huohuo lazima tukubali taasisi/mashirika ya umma sasa hivi yanagombania vipaji na watu wenye uweledi (exceptional expertise) na sekta binafsi hivyo katika uchumi wa kisasa mashirika ya umma yanapaswa kuweka uwiano kati ya kufanya biashara na kutoa huduma(public service)wakati huohuo.
Tumeona mashirika makubwa ya serikali kama TTCL, TRL, ATCL n.k yakishindwa kujiendesha kwa faida au kupanuka hivyo kuendelea kuitia hasara serikali.
Ukosefu wa watu wenye uweledi na uzoefu wa kibiashara ikitajwa moja ya sababu zinazochangia anguko hilo.Jaribu kuona mfano wa shirika na nyumba la taifa NHC kabla ya kuingia mkurugenzi mkuu Bw.Nehemia Mchechu mwaka 2010 akitokea benki ya CBA lilikua halijiendeshi kisasa likitegemea kodi za pango katika majengo yake ya kizamani yaliyokuwa yanageuka magofu kila uchao. Pia kituo cha TIC kabla ya mama Kairuki(rejea maelezo ya Mizengo Pinda mwaka jana ktk ufunguzi wa mradi wa Hallotel) na mifano mingine mingi.
Wengi wa watu wa aina hii(wachache) wenye vipaji na uzoefu katika uendeshaji wa biashara katika sekta husika kwa miaka ya nyuma walikua wanavutwa zaidi na sekta binafsi wakiacha mashirika ya serikali yakiambulia watu wenye weledi wa kawaida kwa kigezo cha maslahi duni.Kwa maoni yangu kupima ughali wa stahili anazopata mtumishi ni sahihi zaidi kupimwa kwa wajibu wake (responsibilities) na uzalishaji wake(output).
Jaribu kufikiri tunahitaji kufufua shirika letu la ndege halafu ikatokea mkurugenzi mtendaji wa Kenya airways ni mtanzania itakua vibaya tukijaribu kumshawishi aje asaidie kulifufua na kuendesha ATCL hata kama atahitaji maslahi makubwa? Kuna maana gani kuajiri mkurugenzi asiye na utaalamu na uzoefu wa kutosha(corporate experience)ukamlipa maslahi ya kawaida(kwa nafasi yake) mfano Tsh.mil 15 akaua shirika lenye mtaji wa mabilion ya fedha au kumlipa mbobezi million 25 akaliendesha kwa faida na kulikuza?
Shirika likiendeshwa kwa faida uwezekano wa kulipa maslahi mazuri kwa wafanyakazi wa kada za chini unakua mkubwa hivyo lengo la usawa hutimia bila kuathiri utendaji.
Kwahiyo dhamira nzuri ya kuweka usawa na kupunguza matumizi isiwe kwa gharama ya kuua mashirika yetu.
Ukweli ni kwamba watumishi hawa ni wachache ambao huajiriwa kwa mikataba ya muda maalumu kukiwa na uchaguzi (option) ya kuongeza kulingana na tathimini utendaji wao.
Hivyo njia sahihi ni kuwa makini wakati wa kuingia mikataba na kulipa kutokana na mchango uliotarajiwa na unaotolewa.
Tuendelee kubana kadri inavyofaa maslahi(kimalipo) ya wanasiasa kwani ni nafasi za wito na uwakilishi wa wananchi....!