Dhambi ya fedha inatafuna siasa-Mzindakaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dhambi ya fedha inatafuna siasa-Mzindakaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jul 16, 2010.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,827
  Trophy Points: 280
  Dhambi ya fedha inatafuna siasa-Mzindakaya
  Imeandikwa na Ikunda Erick, Dodoma; Tarehe: 15th July 2010 @ 23:00


  MBUNGE wa Kwela, Crisant Mzindakaya (CCM), ameaga bungeni jana na kusema vyama vyote vya siasa, ikiwemo CCM, vimetumbukia kwenye uovu wa dhambi ya namna ya kupata viongozi.

  Alitoa kauli hiyo bungeni jana baada ya Spika Samuel Sitta, kumpa dakika 15 badala ya 10 walizopewa kila mbunge kuzungumza wakati wa kuchangia muswada wa Sheria ya Ubia ya Serikali na Kampuni binafsi wa mwaka 2010.

  Katika salamu, shukrani na ushauri wake, Mzindakaya alisema Bunge lijalo ambalo litakuwa la 10, ni lazima lifanywe la uchumi na sifa njema ya Taifa nje ya nchi ihamie kwenye masuala ya kukuza uchumi.

  “Rasilimali tulizo nazo zinatusuta, tunaposaidiwa na nchi kama Uholanzi ambao wamechota bahari wakapata ardhi ili walime,” alisema Mzindakaya.

  Alisema vitu vyote alivyotoa Mungu, Tanzania inavyo na sio sahihi iwe kwenye hali ya uchumi iliyo nayo leo.

  Alisisitiza kwamba ni lazima nchi itumie sheria kati ya matajiri na masikini, kwani utajiri wa nchi uko mikononi mwa watu 10 ambao alishawasema bungeni.

  “Rudini kwa watu wanyonge, saidieni watu wadogo, hawa wenye pesa achaneni nao, ujamaa utakaokuja baadaye utakuwa wa kuumizana kwa wenye pesa na wale masikini,” alisema Mzindakaya.

  Aliongeza kuwa watoto wanaosomeshwa sasa kwa baadaye wanakuwa hawana kazi kwa kuwa uchumi umemezwa na watu wachache, na kwamba serikali itaondolewa madarakani na hao watoto wanaosomeshwa sasa.

  “Tunawasomesha hawa watoto lakini baadaye hawana kazi ya kufanya kwa kuwa uchumi uko mikononi mwa watu wachache, sasa watakuwa mwiba na wataangusha chama tawala,” alisema Mzindakaya.

  Alisema baada ya miaka 15 watakaowaondoa CCM madarakani ni hao wanaosomeshwa leo, kwa kuwa watakuwa hawana cha kufanya.

  Alisisitiza serikali lazima ijenge uchumi wa kati na wa watu wa chini ili kuwa na uwiano wa uchumi, kwani hali itakuwa mbaya ikiwa watu wachache wataendelea kumiliki uchumi.

  Alisema siasa za leo ni fedha, wenye fedha ndio wanaopata ubunge wasio nazo hawana lao na kusisitiza kwamba ni lazima vyama vyote vibadilike viache siasa za fedha.

  “Mimi naondoka bungeni sio kwa uzee, naondoka kwa kujivunia nina akili timamu na bado jimboni watu wananipenda, ninachoomba vyama vyenu vijifunze nidhamu,” alisisitiza Mzindakaya.

  Alisema wakati akiwa kijana na Mwalimu Nyerere alishaapa kamwe hatakubali ubunge kwa kutoa fedha.

  “Nilishaapa nikiwa na Nyerere, sitaki ubunge wa fedha na nilisimamia hilo hadi leo,” alisema.

  Baada ya Mzindakaya kumaliza kutoa shukrani zake, Spika Sitta alimshukuru kwa nasaha zake na kusema, “Nashukuru wewe sio mnafiki, ni mkweli tutaendelea kukukumbuka na maneno yako yatadumu kwa kuwa yanahifadhiwa,” alimalizia Spika huku wabunge walimshangilia kwa makofi.

   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160


  Nadhani wasiwasi wake sio wanyonge, wasiwasi wake ni maintance of the status quo. Miaka yote hiyo imekuwa hivi na amekuwa kwenye utawala kwa muda mrefu sana kwa nini asifanye mabadiliko anayoyasema na anayoyataka yawe na kwa nini akumbuke leo wakati ameondoka?

  Tungemkumbuka zaidi kama angefanya alichosema kuliko kwa kusema ambacho ameshindwa kufanya.
   
 3. M

  Makfuhi Senior Member

  #3
  Jul 16, 2010
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 183
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Maneno yake yanatia moyo lakini angesema kwamba anagombea tena ili asimamie hayo mawazo aliyotoa angeeleweka zaidi. kwa kuwa alishindwa angalau kuyazungumzia hayo kwa miaka 45 aliyokaa bungeni hayana maana.
   
 4. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Angesema hayo akiwa mjengoni angekuwa siyo mwenzao na pengine angenyang'anywa kadi na kuondolewa uanachama wa chama chake. halafu angekula wapi? ingekula kwake na asingepata ile ranchi ya taifa kule kwao
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Jul 16, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Dr. Mzindakaya, bunge na wananchi hawatokusahau kwa mengi uliyofanya, God bless You.
   
 6. W

  WildCard JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Huyu ni mmoja wa watu waloowekeza kwenye SIASA na imewalipa sana. Zitto na wengine endeleeni kumuiga mzee huyu wa Kifipa kwa ile staili yake ya VIBOMU vya hapa na pale na kelele nyingi. Inalipa.
   
Loading...