Dhambi kumi zinazotafuna miili yetu

chrischagama

Member
Apr 26, 2020
7
8
Elimu ni kitu muhimu sana maishani.Ndo maana hata Mwenyezi Mungu alijua kabisa mwanadamu hatoweza kuishi na amani humu dunian ndo maana akatuhasa kumkamata sana elimu tusimwache aende zake.Lakin kwa hapa nchini Tanzania mambo nitofauti kidogo maana jamii inalalamika kwa kuwa wasomi hawajengi taifa lao.Hivi kwa namna hii ya mfumo ndo unategemea maendeleo kabambe nchini.Kwa nchi yetu zifuatazo ni baadhi ya makosa tunayoyafanya na kupelekea elimu yetu kuwa kama ilivyo.

1)Elimu yetu kuwa bidhaa inayonadiwa sokoni.unajua siku hizi mashule kila kukicha yanaanzishwa na mengine hayana hata walimu wenye sifa huoni hata hapo mtaani kwenu kuna kila aina ya shule za awali.Elimu yetu imekuwa sehemu ya watu kujipatia pesa kwa maneno kama hii shule inaufaulu mkubwa ili waweze kuwapata watoto mbalimbali.

2)Elimu yetu inaligawa taifa.Kwa namna gani,unajua kuwa na miongozo miwili tofauti ndani ya nchi moja sio kitu kizur ambapo kuna watoto wa zile shule za changanyikeni ama st kayumba wanasoma kwa lugha ya kiswahili msingi ama miaka saba yote na wakati na wale English medium wakifundishwa kwa lugha za kiingereza.Hivi unadhan mbelen mtu aliyesoma shule za international akubali kuongozwa na mtu anayesoma kwenye hizi shule zetu..huo kama sio ukichaa ni nn hata hao wabunge wanaotumia ujanja na kujenga shule zisizo na ubora wakati watoto wao wanasoma shule za international huku bado tunalifumbia macho yaan toka uhuru bado kuna watoto wanakaa chini bila madawati shukran kwa rais yetu Mheshimiwa Magufuli japo amesaidia kutatua hilo tatizo lkn bado lipo.

3)Elimu yetu kutowajengea wahitimu tabia ya kujisomea vitabu hata baada ya kuhitimu.Unajua wahitimu wetu wa hapa Tanzania wanaona kama elimu ni gereza ndo maana hata wakishamaliza degree zao na kuingia mtaan wanakuwa hawana uelewa sawa na ukimkuta mtu kabahatika kupata kazi hata humo ofisin kukuta kitabu cha hata kujiongezea maarifa hukikuti.Sasa unadhan waliosema good leaders are good readers walikuwa wanamaana gani.Vijana wenzangu wote tujiongeze na kuongeza maarifa ndo maana hata Mungu kupitia biblia anasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.Tuamke tumelala sana tukavune mema ya nchi.

4)Elimu yetu kufundisha wahitimu kuogopa kukosea.Unajua toka shule za msingi yaani ukikosea kidogo unapewa viboko utadhan umemtukana mkuu wa shule,so kwa namna hii tunajenga taifa la watu waoga ndo maana hata katika maamuzi sio rahis kuyafanya.

5) Elimu yetu wengi wanaenda kusomea vyeti baada ya maarifa.Kwa kufanya hivyo unakuta vijana wengi wanakaa mitaan kwa kisingizio cha kukosa ajira ndio hio ni kwel lakin unajua sisi kama vijana tunaenda shule kukaririshwa na kupambana na mitihani kumbe hatujui kama huko mtaani kuna mitahan zaid wakat tunatakiwa tusome kwa uelewa ilimrad hata kijana aweze kujifikiria namna gan kutengeneza kitu flan wengi wa watu wanafanya kazi ambazo hawajasomea.

6)Pia ualimu kuwa kimbilio la wakosefu.Yaan kwa hapa nchin walimu wanaonekana kama watu wa mwisho kabisa waliokosa namna ya kujiendeleza ndo maana weng wanakimbilia huko wakat kazi ya ualimu inatakiwa iheshimike na ithaminike maana wao ndo wanaoandaa watawala na watakaoleta maendeleo kwenye nchi zetu na sio kuwanyima mishahara yaan bora kama kipind hiki cha hili janga la corona walimu wa shule za serikal bado nasikia rais aliamuru walipwe lakini hao kwenye mashule ya binafsi je sijui kama wanapata haki zao maana ualimu watu wanaenda kimkataba hivyo chochote kitakachotokea yeye mshahara wake unatakiwa ubaki palepale hio ndo sheria ya mikataba.

7)Elimu yetu kuzalisha watu wasiohitajika.Unajua kumuaminisha mtu kwamba akishasoma ataajiriwa ni jambo la kusikitisha,Yaan kama serikali yetu ina hamu kutumia maengineer wa kichina hivyo kwann wazalishe maengineer wengine wa kibongo na kuishia kukosa kazi suala la kuwalaumu vijana kwamba hawajui kujiajiri kwanza wewe unaewalaumu hao vijana, wewe umejiajir na wakati sio unahemea mshahara wa serikal huku ukiwa na wasiwasi na penshen ya uzeen.
8)Watanzania tunapuuza vipaji vya watoto wetu.Unajua ili maisha yawe bora panatakiwa pawe na watu wa aina mbalimbali ndo maana Mungu aliumba dunia na mabonde na makonakona mbalimbali hivyo hata jamii yetu inahitaji walau wacheza mpira hapa na huku wanamuziki yaani kila mzazi angefanikisha kipaj cha mwanae jamii ingekuwa na uhafadhali lakin bado tunalia katika umasikin wa kutupa...yaan sikukuu za kiserikal zote Rais angeweka kama utamadun wa shule za aina mbalimbal wakileta ugunduz wao na mshindi atapewa zawad,je unadhan pasingekuwa na ugunduz wa mambo mbalimbali unajua ubongo unaweza fanya chochote unachoamuru ukifanye kuna nguvu katika kufikiri.

9)Pia tunaruhusu kila kiongoz kuvuruga elimu atakavyo.Unajua nyakat tofautitofauti kiongoz akiingia kwenye sekta ya elimu Mara abadilishe grades ziwe hivi Mara mwengine distinction huu sio mpangilio mzuri na wengine kufanya mambo ambayo sio mazur kama 2016 watu form six baada ya mitihan ya taifa kufanywa grade zikaja kubadilishwa hivyo kuleta masikitiko kwa wahitimu...tubadilike.

10)Upatikanaji wa elimu kuwa ni shuruba,karaha na maudhi.Yaan watoto walioshule zetu hizi za kusoma kiswahil masomo yote ndo wanaelewa vizur maana wao ndo wanapitia maneno mbalimbali yaan mtu anamdhihak mwanafunzi kwa kumwambia baba yako ameuza ng'ombe ili aje asomeshe ng'ombe mwengine haya maneno huwavunja moyo wanafunz so kwa upendo tuhakikishe tunajenga taifa letu maana waasisi wetu walijitahidi kulijenga na hivyo pia na sisi tupambane kwa hekima na akili kulijenga taifa letu...Upendo kwa wote Watanzania wenzangu
 
Hapo namba 9 hayo ni maafa yetu, siasa inavuruga sana elimu yetu.
 
Dah inasikitisha...ila vijana wa sikuizi wamerahisishiwa sana mambo shule ziko nyingi sana mm nakumbuka lasaba wakati tunamaliza mwaka 1997 shuleni kwetu walifaulu watu wa 2 tuu na tulikuwa wanafunzi 300 ebu ona...

121.
 
Back
Top Bottom