Dewji ataka Phiri asimamishwe Simba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dewji ataka Phiri asimamishwe Simba

Discussion in 'Sports' started by kilimasera, Mar 28, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MWANACHAMA wa klabu ya Simba, Azim Dewji ameitaka klabu hiyo kutouvumilia utovu wa nidhamu unaofanywa na kocha wao mkuu Patrick Phiri na badala yake amependekeza asimamishwe.

  Dewji, mfadhili wa zamani wa klabu hiyo aliyeifikisha fainali za Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mwaka 1993, ilipotolewa na Stella Abidjan ya Ivory Coast alisema hayo juzi jijini Dar es Salaam alipokuwa anazungumzia uwezekano wa klabu yake kuitoa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huu.

  Klabu hizo zinakutana mwishoni mwa wiki katika raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa na katika mchezo wa kwanza, Simba iliteleza kwa kufungwa mabao 3-1, lakini sasa ikijiandaa kujibu mapigo katika mchezo wa marudiano mwishoni mwa wiki hii.

  Alisema: “Nilikuwa kule Lumbumbushi kuiongezea nguvu, tulifungwa, lakini Mazembe wanaweza kufungika. Lakini, kwa staili hii ya kocha Phiri (Patrick) mtafanyaje vizuri?

  “Kule niliona mapungufu kadhaa kama ilivyokuwa kwa viongozi, wachezaji na mashabiki wa Simba wengine. Kama kocha angeendelea na programu yake kwa wakati, timu ingekuwa imeshakaa sawa, lakini angalia, kocha bado yuko kwao Zambia wakati timu iko vitani, tena na wazoefu kama Mazembe, inashangaza sana!”

  Dewji aliongeza kuwa kwa kocha anayeipenda kazi yake, kamwe asingethubutu kuitelekeza timu kwa karibu wiki moja katika kipindi cha maandalizi ya mchezo muhimu wa marudiano dhidi ya Mazembe.

  “Nakuambia, kwa kocha anayeipenda kazi yake, siku mbili alizopewa zingemtosha na kurejea, lakini amejiongezea siku hadi wiki. Katika suala la nidhamu, wachezaji wajifunze nini kutoka kwake?

  “Naushauri uongozi kwamba ili kuweka nidhamu ndani ya klabu, akirejea Phiri asimamishwe hadi baada ya mechi na Mazembe. Angekuwa na uchungu angekuwa na timu kuipika zaidi na zaidi, lakini hajaonyesha kujali zaidi ya kuwapiga danadana viongozi,” alisisitiza Dewji.

  Baada ya kuteleza kule DRC, Simba inatakiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo ujao Jumamosi ili iendeleze rekodi ya kuwavua ubingwa wafalme wa soka Afrika, kama ilivyokuwa kwa Zamalek ya Misri mwaka 2003.
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Decision point!
   
 3. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #3
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,403
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  sikuwa najua kama Dewjin nae ni kocha.
  ya nini kuajiri kocha toka nje wakati Dewji yupo.? kocha akianza kuingiliwa ndio mwanzo wa kuua timu.
  hebu dewji kua kidogo
   
Loading...