Dereva wetu safari bado, mbona umepunguza speed?

harakat

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
2,888
1,347
Ni asubuhi nyingine na mapema nimeamka natafakari mustakabali Wa Tanzania yetu.

Wakati Wa kuhakiki watumishi hewa kuna Mkuu Wa Mkoa alipewa taarifa zisizo sahihi Mama Kilango alijikuta anatumbuliwa On the spot. Kwa kweli iliwavutia watanzania kwa kasi ile isiyomithilika wala haikuhitaji mjadala mrefu.

Kwa hili kila mmoja aliona kweli tunaiendea Tanzania ya ndoto zetu sasa ni kama mwaka umepita Mama yule alisharudishwa na anaendelea na majukumu ya kulitumikia taifa hili sehemu nyingine .

Tunajiuliza hii haina tofauti na lile la MTU akivurunda Kigoma kaskazini kujamishiwa Kigoma kusini ?

Wakati hatujapata majibu kuna huyu Mh. Wako hapo usoni mwa Kasri lako hapo Ikulu yaani kila uchao ni tuhuma zimepandiana akama santuri za DJ Wa marehemu Pepe kale.

Ikumbukwe tulianza kusafisha watumishi hewa kwa kasi mno .pamoja na hilo vyeti feki ulikua ajenda muhimu na baadhi ya waliobainika sasa hivi wapo sehemu husika wakipata adhabu zao na wengine kesi zikiendelea.

Achilia mbali wale ambayo bado vyeti vyao vipo na vyombo husika uchunguzi ukifanyika huku tayari wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi.

Katika taifa lenye watu zaidi ya Milioni 50 sitegemei hata kidogo kwamba wateule Wa Rais wawe na tuhuma zozote . Hii ni kwa kuwa walifanyiwa vetting ya kutosha kama ulivyotuhakikishia wakati ukiwaapisha wakurugenzi na wakuu Wa wilaya .

Tuhuma za namna yoyote dhidi ya mmoja kati ya wateule wako tunategemea zitolewe ufafanuzi mapema ili kuendelea kulinda si tu hemshima yako kama Rais Wa Nchi yetu Bali pia heshima ya ofisi ya Urais kwa ujumla wake.

Kasi yako ilikua si ya kutilia shaka hasa kwenye kuchukua hatua za kulinda maslahi ya Nchi yetu . Kwa sasa kasi hiyo imeigia nini wananchi wanapaza sauti bado husikii hata kidogo.

Ni kweli mteule wako amekua mstari Wa mbele kwenye kupambana na madawa ya kulevya ila pia kumbuka vyeti feki pia ni ajenda iliyoko mbele yetu .Bado ni suala linaloendelea kuiletea shida taifa letu hasa kwenye utendaji.

Namkumbuka yule mteule wako waliyemtuhumu kuwa na vyeti vya Hotel Management hukusita kumwambia aweke vyeti vyake na wala yeye hakuchukua muda mjadala ile ukaisha .

Sasa huyu Wa sasa kuna nini kinaendelea ?

Vyeti vyake vina uzito gani kiasi kwamba inachukua muda mrefu kuviweka hadharani?

Halafu kama ikiwa kweli huyu ana vyeti feki je waliofanya vetting tutaendelea kuwaamini?

Najiuliza kama huyu Wa usoni ikiwa ni kweli je hawa Wa mbali turudie vetting?

Nimeendelea kutafakari hilo la vyeti je ndio linaleta haya ya kuvamia kituo cha redio?

Je ndio inaleta hisia za kulia kanisani?

Na kweli Rais wangu ndio wewe umekua kimnya kwa tuhuma za mteule wako kiasi hiki??
 
Wa mbali walitumbuliwa malema.. Subiri tuhamie dodona ndio tutumbue Dar
 
Huyo ndo hirizi ya JPM akimtumbua huyo basi vitendo anavyofanya Bashite atavifanya yeye live
 
Back
Top Bottom