Dereva wa lori atoroka na shehena ya korosho huko Mtwara

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,793
Reaction score
29,407
Jeshi la polisi mkoani Mtwara linamtafuta mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Saidi Hamisi Kombo dereva wa gari yenye namba za usajili T 954 BZG na tela lake yenye.no T 397CCY aina ya Scania kwa kosa la kutoroka na shehena ya korosho magunia 405 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia moja na 22 mali ya kampuni ya Starnuts Company Limited.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara Thobias Sedoyeka amesema tukio hilo limetokea eneo la maghalani kata ya Malopokelpo wilaya Tandaimba mkoani Mtwara.

Amesema dereva huyo alikabidhiwa magunia hayo ili kuyasafirisha kwenda bandari ya Mtwara lakini mtuhumiwa huyo alitoweka mara tu baada ya kuingia mtwara mjini.

Hata hivyo amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa namba za gari alizotumia mtuhumiwa ni bandia kwani namba hizo ni za gari aina ya Isuzu Carry na namba halisi za gari hilo ni T 852 APL na tela lake ni T 198 AKY mali ya Gulled Transport LTD inayomilikiwa na Abdi Hers wote wakiwa wakazi wa Dar es Salaam.

Kamanda amesema juhudi za kumtafuta zinaendelea na kutoa wito kwa wakazi wa Mtwara kuwa makini na wezi na matapeli hasa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka ambapo vitendo vya hali hiyo vimekuwa vikiongezeka.

Chanzo: ITV
 
Wizi mwingine ni wa kijinga sana, sasa hizo korosho atazificha wapi na atauzia wapi
 
Dah..Nasikia korosho mbichi zinaongeza pumzi kwa wanaume...atakuwa amezitafuna sana ...anawapanga tu huko aliko. Nimesikia tu mimi 😀😀😀😀
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Huyo dereva hadi kutumia namba za bandia alikuwa tayari ktk mipango ya wizi naami hata jina alilotumia siyo lake
 
Uyo atakuwa kashazihifadhi kwenye maghala maana inavyooneka alishaandaa mazingira mpaka kaweka plate no bandia
 
Dah..Nasikia korosho mbichi zinaongeza pumzi kwa wanaume...atakuwa amezitafuna sana ...anawapanga tu huko aliko. Nimesikia tu mimi 😀😀😀😀
Ha ha ha yaaani zote hizo kwa kuzitafuna tu.
 
Wizi mwingine ni wa kijinga sana, sasa hizo korosho atazificha wapi na atauzia wapi
Watu wameficha makontena, Twiga kapanda ndege, leo unajiuliza kagunia ka Korosho. Au ndio umeingia leo Tanzania ndugu yangu.?
 
Back
Top Bottom