Dereva wa bodaboda auawa kwa mapanga

Dereva wa bodaboda auawa kwa mapanga

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427
MKAZI wa Kata ya Nyahanga Halmashauri ya Mji wa Kahama, Eliud Johnstone (30) ambaye ni mwendesha pikipiki (bodaboda), amefariki dunia baada ya kushambuliwa kwa mapanga na watu wasiojulikana.

Baadhi ya madereva bodaboda walisema kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia juzi katika eneo la Nyakato kata ya Nyasubi na inadaiwa ameuawa na watu wawili waliojifanya abiria ambao baada ya kutekeleza mauaji hayo, walichukua pikipiki yake.

Eliki Elia, na Juma Musa ambao ni madereva wa bodoboda walisema tukio hilo wamelipokea kwa masikikitiko makubwa kutokana na kwamba mauaji hayo yalikomeshwa na serikali ya wilaya ya Kahama kwa muda mrefu sasa.

Mwenyekiti wa waendesha bodaboda ya Kahama (Udapi), Idsam Mapande, alisema taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kwenda kwao, Kasulu mkoani Kigoma zinaendelea kufanyika.

Mapande alisema kwa sasa wanaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuwabaini wahusika wa tukio hilo na aliwataka bodaboda kuwa na subiri pamoja na kuwa makini pindi wanapopata abiria hasa nyakati za usiku na kwamba watembee wawili wawili kama wana shaka na abiria.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Mji wa Kahama na kwamba jeshi la polisi wilayani Kahama limefika eneo la tukio na uchunguzi unaendelea kufanyika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule, alisema jeshi lake litatoa baadaye taarifa ya tukio hilo ingawa uchunguzi unaendelea.
 
Duh Mauaji Ya Kuhusisha Bodaboda Hayaachi Kuripotiwa. Kuna Nini Kwenye Bodaboda?
 
Acha izo mkuu kuwa na hekima Kila siku bodaboda wanaumizwa, wanauawa na kuchukuliwa pikipki zao bila sababu na abiria baadhi ndo wanaofanya michezo ya kuwaingza matatani, Je ni Nani asiejua hili? Mda mwingine uwe unafkiria sio unaongea tu ili mrad!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Wizi wote siku hizi bodaboda zinahusika
 
Back
Top Bottom