Dereva azidiwa kasi na mwanaye

JOSE MOURINHO

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2013
Posts
231
Reaction score
74
Dereva bingwa wa mbio za magari nchini Sweden anayefahamika kwa kuendesha gari kwa kasi, alishindwa kumwahisha mkewe mjamzito hospitali na kufanya mtoto wao kuzaliwa ndani ya gari wakiwa njiani.

Mke wa dereva huyo Per Gunner Andersson alipatwa na uchungu wa uzazi usiku wa manane siku ya Ijumaa, na wakalazimika kwenda hospitali kwa kutumia gari yao aina ya BMW. Bwana Andersson akiendesha kwa kasi yake, alizidiwa kasi na mwanaye. Wakiwa njiani, wawili hao waliona hawawezi kuwahi hospitali, na hivyo kusimamisha gari lao na kupiga simu kuomba msaada wa hospitali. "Nilikuwa mtulivu kabisa" amesema Andersson akizungumza na gazeti la kwenye mtandao la Expression.

Gari la wagongwa liliwasili muda mfupi tu kabla ya mke wa dereva huyo kujifungua mtoto wa kiume. Kutokana na panda shuka hiyo, dereva huyo amesema uenda mwanaye pia akawa dereva wa magari ya mashindano. Andersson alikuwa bingwa wa dunia wa mbio za magari kwa vijana mwaka 2004 na 2007.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…