Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,660
- 1,801
Hili halijazungumziwa ingawaje lina athari kubwa kwa Watanzania waliopo na wajao. Wakati miaka ya themanini deni letu lilikuwa bilioni 7 USD lilitushinda kulipa. leo hii deni letu linakaribia bilioni 30 USD, bado halijazungumziwa. Ni kweli uchumi wa Tanzania umepanuka, lakini pia deni hilo limepanuka haraka hata kushinda uchumi wa nchi.
Tutalilipaje deni hili? Hasa ukiangalia aghalabu madeni haya ya riba huzidi na nadra kupungua. Ongezeko dogo tu la thamani ya dola hivi karibuni kuishalifanya deni hilo kuvimba zaidi.
Nakuapia wazungu safari hii hawatasamehe baada ya kuona upuuzi tulioufanya baada ya kusamehewa. Tumekuwa kama watoto wadogo, kila ukipewa peremende waimaliza haraka ukitarajia kupatiwa nyingine!
Kulikuwa na umuhimu gani wa kuchukua deni kubwa kiasi hicho katika miaka michache tu (2005-2015).
Mtu mwenye akili anapochukua deni analifanyia kitu cha kuzalisha ili kilipe deni hilo, siyo kujenga shule!
Ningependa deni la taifa lijadiliwe, tuambiwe ni kiasi gani, linakuwa kwa kiasi gani kila mwaka na tutalilipaje?
Jamani, si sisi wenyewe tuliomba uhuru kuwa sasa tuna 'akili' za kuendesha mambo yetu? Ndiyo hivi?