Deni la Taifa Lapungua Kwa Dola Milioni 726 Kufuatia Kuimarika Kwa Shilingi

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,110
49,826
Kwa mujibu wa habari iliyonukuliwa na gazeti la The Citizen kutoka kwenye taarifa za Benki Kuu zinazoishia mwezi August zinaonyesha kuoungua kwa deni la Taifa.

Deni la Taifa limepungua Kwa $726 Milioni kutoka $29.52 Bilioni Hadi $28.61Bilion Kufuatia kubadilika bafilika Kwa viwango vya kubadilisha Fedha ikiwemo kuimalika Kwa Shilingi.
20231018_063917.jpg


My Take
Chadema Watapinga,Watasema Samia amekopa sana 🤣🤣🤣🤣.
 
The U.S. dollar has depreciated against other currencies and not really that the TSH has gain value. The big brother knows very well how to play financial game. It Is just a matter of time dollar will come back strong.
 
Naona kama CONTRADICTION

Hali hiyo ina athari hasi katika uchumi wa nchi kwa sababu hivi sasa inahitajika shilingi nyingi zaidi ili kupata Dola ya Marekani.

Mpaka jana Agosti 22, 2023, wastani wa kiwango cha ubadilishaji wa dola kilikuwa Sh2,439.67 kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), huku bei kwa baadhi ya maduka ya fedha, kiwango cha ubadilishaji kikiwa kikubwa zaidi hadi kufikia Sh2,550.

Kitaalamu, ongezeko lolote la kiwango cha kubadilishia fedha za kigeni kinaongeza mzigo wa kulipa kwa Serikali, kwani deni la nje kwa sehemu kubwa lipo katika sarafu ya Dola, hivyo zinahitajika dola nyingi kuendelea kulihudumia.

Hadi mwisho wa Juni 2023, deni la Taifa lilifikia takriban dola 42.44 bilioni (Sh103.5 trilioni). Asilimia 70.7 ya deni hilo sawa na dola 30.01 bilioni ni deni la nje.

Ripoti ya tathmini ya uchumi ya kila mwezi ya Benki Kuu kwa Julai, ilibainisha kuwa muundo wa deni la nje kwa kiasi kikubwa lipo katika Dola ya Marekani, ikiwa ni asilimia 66.9 sawa na dola18.27 bilioni.

Kwa kuzingatia kiwango cha ubadilishaji cha Sh2,334.3 kwa Juni, deni la Dola lilikuwa na thamani ya Sh42.67 trilioni.

Hata hivyo, kutokana na thamani ya dola kuongezeka hadi Sh2,439.67 hadi kufikia Agosti, deni hilohilo sasa lina thamani ya Sh44.5 trilioni na kusababisha nyongeza ya Sh1.83 trilioni.
 
Hiyo ndiyo ajabu sasa. Dollar iko juu halafu tunaambiwa deni la nje linapungua.

Mhariri wa The Citizen ana shida
Ninachoandika ni opinion yangu tu, inawezekana shilingi ikawa strong vs other currency ambayo ikiwa converted to dollar inashusha bei.

Mfano, shilingi ya Kenya Ilikua ni zaidi ya Sh 20 ila sasa hivi ni 16 ksh, Assume Kenya walikua wanatudai Ksh Bilioni 20 hela yetu Ilivyo panda thamani deni litashuka hadi Bilioni 16, hata uki factor hela yetu kushuka thamani vs USD bado deni litashuka
 
Ninachoandika ni opinion yangu tu, inawezekana shilingi ikawa strong vs other currency ambayo ikiwa converted to dollar inashusha bei.

Mfano, shilingi ya Kenya Ilikua ni zaidi ya Sh 20 ila sasa hivi ni 16 ksh, Assume Kenya walikua wanatudai Ksh Bilioni 20 hela yetu Ilivyo panda thamani deni litashuka hadi Bilioni 16, hata uki factor hela yetu kushuka thamani vs USD bado deni litashuka
Mchanganuo wa deni la Taifa unaonyesha karibu nusu ya deni lote la nje linadaiwa na taasisi za kimataifa, ikifuatiwa na wadau wa kibiashara, huku fedha nyingi zikitumika kufadhili miradi na shughuli za miundombinu ya usafirishaji, mawasiliano, ustawi wa jamii, elimu, nishati na madini.
 
Haina maana ikiwa mikesi yoote wanalipa mi bilioni ya dollar kama fidia. Deni la taifa linapungua, madeni ya makesi yanaongezeka.
 
Back
Top Bottom