Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Lengo la mada hii, nikueleza kwa uchache, ni kwa nini demokrasia haijaweza na haitarajiwi kuwa na matunda ya kuridhisha Tanzania katika siku za karibuni?
Wakuu, Mtaji mkuu wa demokrasia ni watu kwa maana kwamba mawazo ya walio wengi yaongoze wakati mawazo ya walio wachache yakiheshimiwa.
Sasa tatizo linalojitokeza kwenye demokrasia ni kwamba, si lazima mawazo ya walio wengi yawe ndio sahihi. Kuna wakati unaweza kukuta waliowengi wanaunga mkono kitu ambacho sio tu kwamba si sahihi bali ni hatari. Hii inasababishwa amma na jamii husika kutokuwa na elimu ya uraia, kutokuwa na taarifa za kutosha kuhusu wanachokiunga mkono au kukikataa au kuwa na taarifa zisizo sahihi au mtizamo/ mzuka hasi.
Tatizo hili ni kubwa sana Tanzania.Tuna watu wengi sana ambao wanaunga mkono au kupinga vitu; ukiwauliza ni kwa nini hawana majibu. Kuna watu wengi sana wanaopenda vitu visivyo na faida kwa jamii kuliko vyenye faida. Pia kuna watu wengi sana wanaotamani kusikia taarifa za watu wengine kufeli au kupata matatizo kuliko wanavyopenda mafanikio yao wenyewe. Jaribu kufikiri demokrasia kamili katika mazingira kama hayo; matokeo yake yanaweza kuwa nini?
Ili hoja hii ieleweke vyema, tutajaribu kutoa mifano miwili.
Jaribu kufikia mkutano wa siasa wenye wagombea wawili. Mmoja akasimama akaongea hoja za msingi sana kwa nusu saa. Mwenzake akasimama na asiongee kitu, akaenda akafungua mziki akaanza kuzungusha kiuno kwa muda wa robo saa tu, kisha akaenda zake kukaa, Unadhani nani atakayeungwa mkono zaidi? Anyway, tuachane na mfano huu labda unaweza ukaleta matokeo mchanganyiko.
Jaribu kufuatilia mijadala hapa JF, kati ya mijadala yenye hoja muhimu ambazo zinaweza kuwa na manufaa makubwa kwa taifa, au mijadala inayojadili watu, ni ipi yenyewafuatiliaji wengi? Bila shaka utabaini kuwa walio wengi wanafuatilia zaidi mijadala inayohusu ubaya wa watu wengine hasa inayolenga kuwadhalilisha wahusika. Hebu fikiria matokeo ya demokrasia kamili katika mazingira hayo!
Kwa mantiki hiyo, demokrasia ni kitu kizuri lakini inaweza kuwa na faida ikiwa tu jamii husika inajitambua, ina uelewa wa kutosha juu ya uraia na mtizamo chanya juu ya vitu ‘Positive altitude’. Vinginevyo demokrasia sio tu kwamba haitakuwa na mafanikio ya maana kwenye nchi husika, bali pia inaweza kuwa hatari kuliko tunavyofikiria kwa sababu inaweza kuwaingiza madarakani watu wa ajabu sana.
Ndio maana baadhi yetu tunafikiri kwamba, kujenga uelewa na mtizamo chanya kwa jamii ndilo jambo la msingi kabla ya demokrasia yenyewe na tukilifanikisha hilo, demokrasia itajiweka mahala pake yenyewe. Tunaweza kusema uelwa wa jamii na mtizamo chanya juu ya vitu ni ‘Major’ na kisha ‘Demokrasia ni ‘Minor’.Vinginevyo ni sawa na kukazana kujenga ghorofa juu ya puto?