ze kokuyo
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 7,417
- 9,603
Jeshi la Marekani lipo kazini kujaribu mfumo mpya kabisa kwa ajili ya ndege yake B-2 stealth bomber.
Mfumo huo ujulikanao kama Defensive Management System (DMS) ni maalumu kabisa kwa ajili ya kuifanya B2 bomber kutambua mahali ilipo mizinga ya kutungulia ndege(SAM) ikiwa kabla haijafika karibu yake. Watengenezaji wa mfumo huo wanasema kwamba utaongeza ufanisi wa ndege hyo hasa katika anga zenye ulinzi wa mizinga ya kisasa ya kutungulia ndege kama S300 na S400.
Pia wameeleza kwamba mfumo huo utasaidia katika kufanya jeshi hilo kupata taarifa nyingi kuhusu utambuzi na mahali ilipo mizinga ya kutungulia ndege na kuongeza ufanisi wa B-2 kupenya kwenye mifumo hyo.
Pia kampuni ya BAE ikishirikiana na Norhrop Grumman wapo mbioni kufunga mifumo mingine mipya kwa ajili ya mashambulizi ya kieletroniki kwa ndege zote 20 za B2.Mfumo huo mpya wa Electronic Support Measure (ESM) system unatarajia kuchukua nafasi ya ule wa zamani wa AN/APR-50 system.
Mifumo mingine inayotarajia kufungwa kwenye B-2 ni ikiwemo ile ya kuweza kurusha bomu la kisasa la nyuklia B-61,makombora ya masafa marefu ya nyuklia, makombora ya masafa marefu yasiyo ya nyuklia, makombora ya kuharibu mizinga ya kisasa ya kutungulia ndege,nk.Maboresho haya yanafanywa kuongeza ufanisi wa ndege hyo B-2 bomber ikiwa ni kutokana na kuongezeka kwa mizinga ya kisasa ya kutungulia ndege kama vile S300 na S400.
Mpaka sasa B2 bomber imefungwa processor mpya kabisa ambazo inaarifiwa kwamba imeongeza uwezo wa ndege hyo zaid ya mara elfu moja.Moja ya kazi ya processor hzo ni kuongeza ufanisi wa silaha katika kupiga vitu husika.
Nia ya maboresho haya ni katika kuongeza ufanisi wa ndege hyo pia kuongeza muda wa ndege hiyo kuendelea kufanya kazi zake kisasa(kidijitali) zaidi hadi mwaka 2058.