Definite Truth!

Definite Truth!

decomm

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2013
Posts
726
Reaction score
668
Kwamba ipo siku utakufa.
Sote tutakufa.
_____
Amani iwe kwenu.

Huu ndiyo ukweli usiopingika, uwe mwenye imani kuwa Mwenyezi Mungu yupo au la, siku itafika utakufa.

Ule vizuri, ufanye mazoezi, ufanye yote utakayoweza hapa duniani lakini ipo siku utakufa.

Kifo ni mawaidha mujarabu kwa wenye imani na uwepo wa Mwenyezi Mungu.

Tujitahidi kuacha kufanya mabaya na tujitahidi kutenda yaliyo mema na kufanya ibada mbalimbali.

Katika mitihani ya masomoni huwa tunapewa maswali na muda lakini tunafichwa majibu, ila katika maisha ya imani za kidini 'tumepewa maswali na majibu', lakini tumenyimwa muda!

Tuwaidhike (lets take heed)

Hatujui siku wala saa.

Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwa hakika kwake tutarejea.

decomm!
 
Kifo ni kipimo cha imani kwetu wanadamu tunajisahau sana.
.
Mshahara wa dhambi ni mauti.
 
Lakini ukweli ni kwamba wote wafao hawajui kwamba wamekufa na huwaona waliobaki wakihangaika kutokana na "kifo" cha mpendwa wao kwa mshangao mkubwa!
 
Lakini ukweli ni kwamba wote wafao hawajui kwamba wamekufa na huwaona waliobaki wakihangaika kutokana na "kifo" cha mpendwa wao kwa mshangao mkubwa!
Kwa imani za dini, wanajuwa.

Wanajuwa pale Malaika wa mauti awajiapo.

Kuna maisha baada ya kifo, ubora wa maisha hayo hutegemea imani matendo yako hapa duniani, pia Rehema ya Mwenyezi Mungu.

decomm!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom