Kama kweli umeamua sioni hata kwanini upoteze muda wako kumuambia wewe sio mamlaka ya hali ya hewa. Anajua kua wewe sio mamlaka ya hali ya hewa toka anapokuambia its raining.
Kaa kimya, huna sababu ya kujibu chochote. Kuna watu wako smart, unamjibu wewe sio mamlaka ya hali ya hewa anakuja na lingine, unaendelea kujibu, mwisho umeingia kwenye 18 zake.
Kama umeamua futa mawasiliano na huyu mtu huna sababu ya kujibu msg yake hata moja, labda akueleze habari ya msiba ya mtu ambae na wewe ulikua unamfahamu.
Mwanzo wa kujibu msg moja ndio muendelezo wa nyingine, hata akituma msg zaidi ya 10 wewe kimya maana umeshaamua, ita click kua "kimenuka" labda awe zezeta.