DED Korogwe akalia kuti kavu

DED Korogwe akalia kuti kavu

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,606
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba amempa saa 24 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Vijijini, Khalfani Magani kujieleza kwa nini asichukuliwe hatua za kinidhamu kwa madai ya kuficha fedha za mfadhili za ujenzi wa shule.

Agizo hilo amelitoa jana Alhamisi Septemba Mosi 2022 wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Mgwashi iliyopo wilayani Korogwe, akimtaka kiongozi huyo ajieleze kwa nini asiondolewe kwenye nafasi yake hiyo.

Mgumba amesema kuwa ameamua kutoa maagizo hayo baada ya mkurugenzi huyo kuchelewesha ujenzi wa shule ya sekondari Mgwashi uliokuwa ukamilike Juni mwaka huu.

Mkuu wa Mkoa huyo amesema shule hiyo ilipatiwa mgao na Serikali wa Sh600 milioni ambapo awali walipokea Sh470 milioni huku mfadhili alishatoa zaidi ya Sh100 milioni kwaajili ya ujenzi huo lakini Mkurugenzi huyo hakutaka kueleza taarifa hiyo ya Mfadhili kwenye kikao chochote.

"Umeletewa fedha mwezi wa 12 (Desemba) na huu mradi ulitakiwa ukamilike mwezi wa nne (Aprili), kuna watu walikuwa na nia ovu ya kumchonganisha Rais (Samia Suluhu Hassan) na wananchi wa Mgwashi hatutawavumilia na hawana nafasi kwenye utawala huu," amesisitiza Mgumba.

Ameongeza kuwa, “Mkurugenzi nataka ujieleze ndani ya masa 24 kwanini umechelewesha mradi na kwamba majibu yake kama yatanidhisha ndiyo nitamshauri Rais au Waziri hatua gani za kufanya na tabia ya kuchelewesha mradi iwe mwanzo na mwisho.”

Mgumba amesema miradi ikicheleweshwa hauna ufanisi wala gharama halisi ya fedha na pia inakuwa imecheleweshwa huduma kwa wananchi.

Mbali na mkurugenzi huyo kutakiwa kujieleza lakini pia aliagizwa kuanza kulipwa a fidia leo kwa wananchi 48 waliokuwa wanalima kwenye eneo hilo ambalo linajengwa shule hiyo ya sekondari.

Kwa upande wao wananchi wamesema kuwa kukosekana Kwa shule ya sekondari kulikuwa kunasababisha utoro wanafunzi kwani shule waliyokuwa wanategemea ilikuwa na umbali wa kilometa 5 hadi 10.
 
Sasa mkurugenzi mwenyewe usikute alikuwa ni Uvccm na kadigrii kake ka sociology huko!

Kutokana na ukada wake ndani ya chama, kufahamiana na baadhi ya wakubwa wa Lumumba, kapewa Ukurugenzi! Halafu tutegemee maajabu!!!
 
DED wa Korogwe aende tu pale Kwasemangube kuna Mtaalam hatari hata Bosi akiwa Mbogo vipi anapoa anakua bariiidi kama tusker.
 
Mwingine ni DED wa Sumbawanga MC, leo tumetoa onyo la mwisho….. bwana mdogo Mtalitinya chuma kikoli-moto.
 
Ukiachana na stendi, miradi yote iko chini ya kiwango na haikamiliki wakati pesa zote alishapewa…. leo RC kamtolea uvivu na sioni anatokaje!
Naujua Mkoa wa Tanga vizuri haswa kwa zengwe lakini huyo wa Sumbawanga ni kweli huenda anayakoroga ni wakati sasa ayanywe.
 
Hivi Kuna haja Gani ya kusomesha Vijana wetu!? Kazi yoyote ya kutumia Hela za Kodi lazima kuwe na usanifu na kuwa na makadirio ya Gharama, Sasa huyo mkurugenzi atatumiaje Hela ya Kodi ya wananchi bila kufuata huo utaratibu!? Value for money itakuwaje kama itajengwa kazi substandard!! Huku ndio wanasiasa wanashibia
 
RC hana mamlaka ya kinidhamu kwa DED kwa vile haripoti kwake. DED anawajibika kwa KM- TAMISEMI.

RC anaweza kushauri tu aondolewe
 
Mkwara tu huu. Tena huyo mkuu wa mkoa ajiangalie. Awamu hii kuna tujitu tuna vyeo vidogo lkn twa moto kweli kweli, ukitutumbua tu unapunguza kibarua chako.

Reference: Kamuulizeni Kafulila
 
DED anafichaje hela kwani hela ni Sindano mpaka afiche!
Hizo hela wakifuatilia vizuri utakuta makada wa chama Twawala wameshafanya yao kwa kumtisha DED!!!
 
Back
Top Bottom