DED Kiteto awatolea uvivu wazazi

JAMHURI

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
449
60
Mkurugenzi mtendaji wa halm ya Wilaya ya Kiteto, Tamim Kambona amevunja ukimya na kuwataka wazazi kutoozesha watoto waliohitimu elimu ya msingi kwa kuwa bado wanaendelea na masomo.

Kambona aliyasema hayo katika maafali za Shule mbalimbali wilayani humo kuwa vitendo hivyo vimekuwa mazoea kwa jamii hiyo.

"Kuna baadhi ya wazazi humu walikuwa wanasubiri watoto wahitimu..nasema wakome hili halitavumilika tutawashughulikia"

Alisema serikali ya awamu ya tano imeweka mazingira mazuri katika elimu ili kila Mtoto Wa kitanzania aweze kupata elimu hivyo kutotumiwa fursa hiyo ni kuwanyima haki yao.

Shule alizofika Mkurugenzi huyo na kutoa ujumbe ni pamoja na Shule ya msingi ya Kimataifa Lalakir, Shule ya Kiperesa, Kaloleni ambapo amesisitiza wazazi na waalimu kutimiza wajibu wao.
 
Back
Top Bottom