Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,504
WAWEKEZAJI na wafanyabiashara wakubwa na wadogo wilayani Muheza mkoani Tanga ambao watagoma kuchangia fedha za maandalizi ya ujio wa Mwenge wa Uhuru katika wilaya hiyo wafungashe vilago kwani watakuwa hawafai.
Hayo yalisemwa juzi na mkuu wa wilaya ya Muheza Esterina Kilasi katika kikao cha cha maandalizi ya ujio wa Mwenge wa uhuru wilayani Muheza kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Muheza na kushirikisha wakuu wa idara, watendaji wa kata, maafisa tarafa na viongozi wa vyama vya siasa.
Alisema mwenge wa uhuru ni kitu muhimu katika nchi hii toka enzi ya Baba wa Taifa hayati Julius Kambarage Nyerere, kwa hiyo alisema wafanyabiashara lazima wachangie pamoja na wafanyakazi na watu binafsi ili kuongeza nguvu
katika ujio wake huku akimuagiza afisa biashara wa wilaya kuorodhesha wafanyabiashara wote ambao hawana leseni ili wachukuliwe hatua.
Kilas alisema kama mwekezaji hataki kuchangia mwenge wa uhuru, aondoke katika wilaya yake kwa kuwa atakuwa hafai kwani mwenge wa uhuru unaunganisha watu kuwa pamoja na kuleta maendeleo ya kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aliwataka maafisa watendaji wa kata na Afisa biashara wa wilaya hiyo kukusanya fedha hizo za maandalizi ya ujio wa mwenge wa uhuru ambao utawasili wilayani Muheza Tarehe 2/5/2016 ambapo utazipitia miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri hiyo.
Source: Nipashe-Jumapili