DC wa Tarime, ni nani atakuamnini tena?

DC wa Tarime, ni nani atakuamnini tena?

Joined
Aug 29, 2016
Posts
21
Reaction score
12
Ni zaidi ya miezi miwili sasa imepita tangu waziri wa Nishati na madini mh Sospeter Muhongo alipotoa maagizo kwa mgodi wa north Mara gold mine (acacial,kuwalipa fidia ya ardhi yao wananchi wanaozunguka mgodi huo,kamati iliyoundwa na mh Muhongo ilipendekeza ifikapo mnamo tarehe 30/09/2016 mgodi uwe umekamilisha ulipaji wa fidia hizo,waziri Muhongo alimuagiza Mkuu wa wilaya kusimamia mapendekezo hayo ili yatekelezwe kwa wakati,hadi inafika tarehe 30/09/2016 mgodi ulikuwa haujatekeleza agizo hata moja la serikali,na wananchi umekuwa wakilalamika mgodi wa north Mara kutumia pesa kupooza ukweli halisi,na hata Mkuu wa wilaya ni moja kati ya watuhumiwa wakubwa juu ya rushwa inayoendeshwa ndani ya mgodi huo,hadi Jana tarehe 10/10/2016 Mkuu wa wilaya alipoitisha mkutano wa ulaghai kuwahadaa wananchi eti anatoa agizo kwa mgodi huo,Mkuu wa wilaya anasema ametoa sasa Siku 20 mgodi kuwalipa fidia wananchi hao,yani ifikapo tarehe 30/10/2016,Mkuu wa wilaya aache usanii,aache kuigiza,aache kuchekesha,Mkuu huyu wa wilaya sasa unakuwa ndo mchekeshaji( comedy), Mkuu huyu anashindwa kumwambia wananchi ukweli kuwa,ni nini kilisababisha mgodi kushindwa kutekeleza maagizo ya kamati ya Muhongo kwa wakati,Mkuu wa wilaya anashindwa kusimamia maagizo ya kamati iliyopendekeza mwisho wa fidia 30/09/2016,sasa Mkuu wa wilaya anageuka kuwa msemaji wa mgodi badala ya kusimamia maagizo ya serikali,Mkuu huyu wa wilaya anachekesha sana,kuna wanaodai eti ameamua kufanya mkutano wa kuwadanganya wananchi ili kuwazubaisha wale ambao wamepanga kuonana na Rais MAGUFULI Mara atakapokuja butiama
 
Back
Top Bottom