Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
WAKATI leo kuanzia majira ya saa alfajiri hadi saa 4 ;00 asubuhi ilikuwa ni siku ya wajinga duniani, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw Richard Kasesela amewakamata wanahabari wawili wa kituo kimoja cha Radio Fm mkoani Iringa kwa madai ya kuchukizwa na matumizi mabaya ya jina lake katika kudanganya umma.
" Ahsante sana nimewakamata waandishi hao wawili kwa kosa moja kubwa ...mwandishi mmoja aliingia studio na kujitangaza kuwa yeye ni mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela na kuanza kutoa ahadi za kupeleka msaada wa mahindi Kipera na ahadi nyingine nyingi na hata kunidhalilisha hata mimi hii ni sikukuu ya wajinga ya kutaniana zaidi na ni kosa kutumia chombo cha habari kutania na ukitumia chombo cha habari kutania basi ukimaliza tu kutania bila hata kupumzika unapaswa kueleza wasikilizaji kuwa hakuna ukweli wa jambo hilo na ilikuwa ni siku ya wajinga.....wao wametangaza kiutania kudanganya watu hata mimi nimewakamata kiutani hivyo hivyo"
'Siku ya wajinga ipo miaka yote ila kujiita wewe ni fulani ama kiongozi na kutumia jina hilo kudanganya watu huo ni sawa na utapeli na upotoshaji .......kwani hata baadhi ya vitu vya kudanganya ni vile ambavyo haviwezi kuhatarisha amani ama kuchafua mwingine kwa kisingizio cha siku ya wajinga....mfano ukatangaza kuwa polisi wameua watu 10 wakati ni utani unafikiri nini ambacho kwa utani wako huo unaweza kuligharimu jeshi la polisi ....wananchi wanaweza kuandamana kwenda kuvamia polisi kwa utani wako."
Alisema kuwa sikukuu ya wajinga ni saa 4 tu na sio zaidi ya hapo na kuwa kutokana na kutangaza uongo huo amepokea simu kutoka kwa waathirika wa mafuriko ambao walikuwa wakilalamika hatua ya serikali kuwaacha walengwa wa chakula cha msaada na kupeleka sehemu ambayo haina shida ya chakula cha msaada hivyo kuvitaka vyombo vya habari kujenga heshima yake kwa kuendesha vyombo hivyo kitaaluma zaidi badala ya kuvitumia kwa upotoshaji.
Source: Mkuu wa Wilaya, Kasesela awakamata waliotumia jina lake redioni kuadhimisha siku ya wajinga.
===========
UPDAATES;
===========
Ufafanuzi:
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, aliwakamata waandishi wa habari wa kituo cha Radio Ebony FM cha mjini Iringa na kuwaachia. Baada ya kuwafikisha kituoni, aliwaambia leo ni Siku ya wajinga(Fools Day), hivyo ngoma droo, akawaachia wakaondoka.