DC Umetuheshimisha"Mwenyekiti wa Wenyeviti wa mitaa Temeke

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
"DC UMETUHESHIMISHA"MWENYEKITI WA WENYEVITI WA MITAA TEMEKE.

Mkuu wa wilaya ya Temeke Mheshimiwa Jokate Mwegelo amefanya kikao na wenyeviti wa mitaa 142 inayounda wilaya ya Temeke, Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Manispaa ( Iddi Nyundo).

Katika kikao hicho wenyeviti wamempongeza mkuu wa Wilaya kwa kuteuliwa kuiongoza Wilaya hiyo na kwa namna alivyo kiongozi shupavu, mwenye juhudi katika kupigania maslahi ya Wananchi.

"Kiongozi wetu ni kijana mdogo mwenye 'focus',hili ni jambo kubwa kuwahi kutokea Temeke, kiongozi mkubwa kukaa chini na wenyeviti ambao ni kama macho na masikio yake,kwa kweli DC umetuheshimisha" Alisema Ndg. Salim Kawambwa, mwenyekiti wa wenyeviti wa serikali za mitaa ya Temeke, ambaye pia ni mwenyekiti wa mtaa wa Kitunda.

Akizungumza mara baada ya kuwasikiliza wenyeviti hao, Mhe. Mwegelo amesema kwamba ushirikiano pamoja na heshima kwenye utendaji kazi ni muhimu katika ujenzi wa Taifa moja.

"Kama nilivyosema mimi ni muumini wa 'team work' naamini katika ushirikiano, tunajenga nyumba moja inabidi tukae,tuongee na tuje na kauli moja thabiti ili kuweza kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wetu" Alisisitiza mkuu huyo wa Wilaya.

Aidha Mhe. Mwegelo amewakumbusha watendaji wote wa serikali kuheshimu kazi, pamoja na kuheshimu mamlaka walizopewa katika kutekeleza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi wa Temeke, ikiwemo kuheshimiana wao kwa wao.

Tangu kuteuliwa kwake, Mhe. Mwegelo amekuwa akifanya vikao na makundi mbalimbali ya viongozi wilayani hapa, lengo la vikao hivyo ni kufahamiana, kufahamu viongozi hao wanataka nini, na vipi ni vipaumbele vyao katika utendaji kazi wao,hii yote ni katika kuhakikisha kwamba anatimiza falsafa yake ya kufanya kazi kwa pamoja 'team work' ambayo amekuwa akiisisitiza katika vikao vyake vyote.

IMG_20210723_164608_845.jpg


IMG_20210723_164608_846.jpg


IMG_20210723_164608_855.jpg


IMG_20210723_164608_849.jpg
 
Back
Top Bottom