DC Ukerewe kuburuzwa kortini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DC Ukerewe kuburuzwa kortini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kibogo, Oct 23, 2012.

 1. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,477
  Likes Received: 784
  Trophy Points: 280
  WENYEVITI wa vitongoji na vijiji wilayani Ukerewe, Mwanza wanaodai posho ya kusimamia Sensa ya Watu na Makazi, wamepitisha azimio la kumshitaki mahakamani mkuu wa wilaya hiyo.
  Wenyeviti hao wa vitongoji na vijiji wapatao 256 walipitisha azimio hilo jana katika kikao chao kilichofanyika mjini hapa.
  Viongozi hao walifikia uamuzi huo baada ya kutoridhishwa na majibu yanayotolewa na Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Mariam Mseleche na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Joseph Mkundi, ambao nao walishiriki kikao hicho.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Wenyeviti wa Vitongoji na Vijiji wa wilaya hiyo, Hussein Hassan, alisema mbali ya azimio hilo pia wamekubaliana kususia shughuli zote za maendeleo na kuongeza kuwa hivi sasa wanawasiliana na wanasheria, ili suala hilo walifikishe mahakamani kwa utatauzi wa kisheria.
  Katika madai yao, kila mwenyekiti wa kitongoji anadai posho ya sh 140,000 pamoja na posho ya madaraka ya kila mwezi ambayo hawajalipwa tangu Septemba mwaka jana mpaka sasa.
  Katika hatua nyingine viongozi hao wa vitongoji na vijiji wametaka posho ya madaraka kwa wenyeviti wa vitongoji iongezwe kutoka sh 5,000 ya sasa hadi sh 35,000 kwa mwezi huku wenyeviti wa vijiji wakitaka iongezwe kutoka sh 10,000 hadi 50,000.
  Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Mariam Mseleche, akizungumzia madai hayo alisema yapo nje ya uwezo wake na kuaidi kuyafikisha katika mamlaka husika.
  Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Joseph Mkundi, ameahidi kufuatilia na kupata ukweli wa madai ya kutolipwa posho ya madaraka na kulipatia ufumbuziWENYEVITI wa vitongoji na vijiji wilayani Ukerewe, Mwanza wanaodai posho ya kusimamia Sensa ya Watu na Makazi, wamepitisha azimio la kumshitaki mahakamani mkuu wa wilaya hiyo.
  Wenyeviti hao wa vitongoji na vijiji wapatao 256 walipitisha azimio hilo jana katika kikao chao kilichofanyika mjini hapa.
  Viongozi hao walifikia uamuzi huo baada ya kutoridhishwa na majibu yanayotolewa na Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Mariam Mseleche na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Joseph Mkundi, ambao nao walishiriki kikao hicho.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Wenyeviti wa Vitongoji na Vijiji wa wilaya hiyo, Hussein Hassan, alisema mbali ya azimio hilo pia wamekubaliana kususia shughuli zote za maendeleo na kuongeza kuwa hivi sasa wanawasiliana na wanasheria, ili suala hilo walifikishe mahakamani kwa utatauzi wa kisheria.
  Katika madai yao, kila mwenyekiti wa kitongoji anadai posho ya sh 140,000 pamoja na posho ya madaraka ya kila mwezi ambayo hawajalipwa tangu Septemba mwaka jana mpaka sasa.
  Katika hatua nyingine viongozi hao wa vitongoji na vijiji wametaka posho ya madaraka kwa wenyeviti wa vitongoji iongezwe kutoka sh 5,000 ya sasa hadi sh 35,000 kwa mwezi huku wenyeviti wa vijiji wakitaka iongezwe kutoka sh 10,000 hadi 50,000.
  Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Mariam Mseleche, akizungumzia madai hayo alisema yapo nje ya uwezo wake na kuaidi kuyafikisha katika mamlaka husika.
  Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Joseph Mkundi, ameahidi kufuatilia na kupata ukweli wa madai ya kutolipwa posho ya madaraka na kulipatia ufumbuzi

  My Take:
  Zoezi la sensa kama tulivyoshuhudia limeishamalizika sasa inakuwaje hadi leo viongozi hawa hawajalipwa? fedha hazikutolewa au kama zilitolewa zimekwenda wapi? na nina mashaka inawezekana kabisa kuna maeneo mengi kuna tatizo hili isipokuwa yale maeneo yenye muhemko wa kisiasa watu ndo wanajua kudai haki zao lakini kuliko lala ndo wamelizwa kimya kimya

  Source ni TANZANIA DAIMA (23 OCT 2012)
   
 2. q

  querauk Member

  #2
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ponda na wenziwe ndo wanatakiwa washitakiwe kwa kuhamasisha waislamu kugomea sensa na siyo DC aliyefanikisha sensa kwa wakerewe kwenye visiwa zaidi ya 50
   
 3. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Sasa hapo DC anahusikeje
   
Loading...