DC Siha, mbunge Mollel waivuruga CCM na Halmashauri ya Siha

Mlokole Mahiri

New Member
Jun 7, 2020
3
22
Mkuu wa wilaya ya Siha ndugu Onesmo Buswelu na Mbunge wa Jimbo Hilo na Naibu Waziri wa Afya ndugu Godwin Mollel wameonekana kuivuruga Halmashauri ya wilaya ya Siha na CCM Wilaya ya Siha kwa kinachoonekana tamaa za madaraka na Vita ya kuwania Jimbo Hilo kwa ajili ya uchaguzi ujao.

Kumetokea mgawanyiko mkubwa Sana kufuatia DC huyo na Mbunge kwa upande mmoja na mwenyekiti wa Halmashauri na baadhi ya viongozi wa ccm Wilaya kwa upande mwingine kuwa kwenye Vita kubwa. Chanzo kikitajwa Ni eneo lililokua linamilikiwa na chuo Cha polisi Moshi (kilele pori )kurudishwa kwa wananchi wa maeneo jirani ambao ndio wamiliki halali lkn DC na Mbunge walitaka kumega eneo la wananchi na kumpa mwekezaji kwa maslahi yao binafsi ambapo mwenyekiti wa Halmashauri ndugu Ngomuo alisimama kidete kuhakikisha wananchi hawadhulumiwi.

Uhasama umezidi mpk kufikia hatua ya mwenyekiti huyo kuondolewa madarakani kwa hila kwa kudaiwa kutetea watumishi walioadhibiwa bila kufuata Sheria huku wengine wakionekana hawana hatia.
Mwenyekiti huyo alipinga kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ikiongozwa na DC huyo kuvamia kikao Cha kamati ya nidhamu ya Halmashauri na kulazimisha maamuzi yao huku ikiwatishia wajumbe kuwashughulikia Kama watapingana na maamuzi yao.

Vyanzo vya ndani vinasema DC huyo anachukua maamuzi hayo kujilinda na tuhuma mbalimbali za kuvuruga ujenzi wa Hospitali ya wilaya yeye Kama mwenyekiti na msimamizi Mkuu wa mradi. DC huyo anatuhumiwa kuhujumu mradi tàngu ilipoanza kazi ya ujenzi wa jengo la NHIF kwa nguvu za wananchi ambapo aliweka fundi wake na wakati huo huo akampa kazi ya kujenga nyumba yake binafsi na kutumia vifaa vya ujenzi vya jengo hilo kujengea nyumba yake binafsi.

DC huyo alikua anakusanya vifaa na fedha yeye mwenyewe kutoka kwa wananchi na makampuni mbalimbali na kupanga matumizi yeye na fundi wake. Fundi huyo alisema alijenga nyumba hiyo binafsi ya DC bila kulipwa baadhi ya malipo yake kwa kuahidiwa kupewa kazi ya kujenga jengo moja katika mradi wa majengo Saba ya 1.5bilioni .


Inasemekana fundi huyo alipewa kazi ya jengo la mortuary bila kuomba zabuni Kama mafundi wengine na mtindo wa kuhamisha vifaa vya ujenzi kwenda kumalizia jengo la DC uliendelea ikiwemo tiles.

Nyumba ya DC ilikamilika na akampa mwanasheria wa Halmashauri akae hapo majengo ya hospital hayajakamilika.


Tuhuma zingine za DC huyo Ni kujifanya mtaalamu wa manunuzi kwa kuagiza vifaa toka kwa wazabuni anaowataka yeye na bila utaratibu na kuamuru wataalam kuandaa nyaraka kuhalalisha manunuzi hayo.

Mfano wa vifaa hivyo Ni tiles alizoagiza yeye kutoka kiwandani na kusababisha hasara kwa Halmashauri. Vifaa vingine Ni mbao, milango, mchanga,nk. Ambapo alikua anaagiza kwa wazabuni wake kwa simu na kuagiza wataalmu wakamilishe order za wazabuni hao.


DC huyo pia anatuhumiwa kutongoza wanafunzi wa A-level wa shule za secondary Oshara na Nuru. Baadhi ya waalimu wa shule hizo wamedai kukerwa na tabia ya DC huyo kufika ghafla me madarasani kwao wakiwa wanafundisha kukaa kwenye dawati na wanafunzi na baadae mwalimu akitoka huwauliza wanafunzi kuhusu ufundishaji wa waalimu husika.

Hatua za ziada inabidi zichukuliwe mapema maana DC huyo ameanza kufukuza Watumishi wazalendo wa Halmashauri ambao wanajua mambo ya hovyo anayofanya.

Ikumbukwe kwamba DC huyu akishirikiana na Mollel ndio walioratibu kuwanunua Madiwani wa Chadema na kuchukua Halmashauri kiharamia. Kumekuwa na malalamiko ya wananchi juu ya viongozi hawa wawili ambao hawana chembe ya uadilifu.

Mtumishi, Siha DC
 
Hapo kwenye kununua wapinzani ndiyo patampa kinga ya uhakika toka kwa mamlaka ya uteuzi na utenguzi!!

Maana hiyo ndiyo kazi rasmi iliyowaweka hapo,kama wameitekeleza kiuhakika basi hayo mengine hayataangaliwa kabisa,sana sana watapandishwa vyeo,ukiweza kupambana na upinzani( hasa chadema) basi hata ukiamua kuchinja raia wema barabarani hutoguswa!!

Hakuna atakayekugusa,mamlaka itakulinda kwa gharama yoyote, huoni Bashite ametuhumiwa hadi na jumuiya za kimataifa kwa kuwanyima watu haki ya kuishi lakini mbeleko ndiyo inazidi kukazwa?

Tulieni tu,mmeshapoteza mchezo hata kabla haujaanza.
 
Hivi Mollel si alitoka huko CHADEMA? Mbona kabla ya apo sikuyasikia aya!!?
 
Nilikua maeneo ya Kilingi na Naibili miezi miwili iliyopita, nilpata kusikia mengi sana yanayoendelea na pia kuna mzee mmoja aliniambia watu wamechoka sasa na mollel amekua mzigo kwa watu

Pia kuna mwalimu aliniambia kwamba wameandika barua kwa afisa elimu kumshtaki huyo DC maana amekua akiingilia kazi za waalimu, na wakati mwingine amekua akiadhibu hadi wanafunzi kila anapotembelea shule

Kiukweli kama hizi tuhuma nilizosikia n ahizi unazoweka hapa ni za kweli basi kazi ipo
 
Wahamiaji maji marefu. Prof Kitila na Mwita wameshapewa onyo. Mollel kapiga debe sana na kuisaga CHADEMA. Eti Lissu alipigwa risasi na CHADEMA By Mollel. Akidhani atapewa donge nono.

Natunza akiba ya maneno mpaka baada ya mwezi wa 10, nikisubiri jinsi Mollel atavyoropoka nami nimalizie maneno yangu.

Nchi hii vyuma vimekaza, vinatupa uchizi wengi.
 
Acha majungu wewe,DC Buswelu siyo wa type hiyo unayotaka awe,acheni kuchafua watu kwa interest zenu za kipumbavu.DC Buswelu piga kazi,usibabaishwe na hao pimbi.Hivi siha yote upo wewe tu wengine hawayaoni unayoyaandika hapa? Wewe ni bacteria?Au ndio unajifunza kuandika insha? Kiufupi, acha majungu ndugu hayatakufikisha popote,piga kazi tu utatoboa kimaisha.
 
Back
Top Bottom