Mwanafalsafamweusi
Member
- Jun 4, 2019
- 14
- 23
Mkuu wa wilaya ya Same Bi.Rosemary Senyamule akiwapokea washiriki wa miss Arusha 2019
Wakuu wa wilaya kwa Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa kwenye Picha ya Pamoja na Warembo.
Mkuu wa Wilaya ya Same Bi Rosemary Senyamule amewakutanisha Warembo wanaoshiriki Miss Arusha 2019 na wakuu wa wilaya wenzake wa wilaya za mkoa wa Kilimanjaro ambao ni DC wa moshi Ndugu Kipre Warioba,DC wa Rombo Agnesi Hokororo ,DC wa Siha ndugu Onesmo Buswelu na DC wa Hai ndugu Lengai Ole Sabaya .Wakuu hao wa wilaya kwa pamoja wamewapongeza warembo kwa namna wanavyojitolea kuisaidia jamii ya watu wanao wazunguka wenye uhitaji maalumu na kuwataka wao kama vijana kushiriki pia kwenye chaguzi za serikali za mitaa na kuwahamasisha vijana wenzao pia.Ikumbukwe kuwa Warembo hao walienda kutembelea hifadhi ya Taifa ya Mkomazi iliyopo wilayani Same kwa DC Rosemary Senyamule yenye Sifa ya Kuwa na wanyama walio kwenye Kundi la Big5 ambao ni Simba,Chui,Faru,Tembo na Nyatina pia walitoa msaada kwa familia yenye watoto watano wenye ulemavu iliyopo Chome wilayani Same.Mkurugenzi wa The Function Hose ndugu Till Chizenga ambae ndie mwenye kamati ya maandalizi ya Kamati ya miss Arusha 2019 amewashuruku wakuu wa wilaya hao kwa kukutana nao na kutoa ushauri kwa warembo hao ambao utawazidishia ujasiri kuelekea kilele cha miss Arusha tarehe 5/7/2019 ambapo pia wakuu hao wa Wilaya wamepokea mwaliko wa kuhudhuria Mashindano Hayo yatakayo fanyika jijini Arusha.Pia amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Hai kwa kuwakaribisha kutembelea wilayani Hai hasa kwenye Chanzo cha maji cha Chemka ambacho ni moja kati ya vivutio vya utalii chenye sifa ya kuwa na maji ya moto muda wote .