DC Same awakumbuka wazee wastaafu

DC Same awakumbuka wazee wastaafu

nyanile

Senior Member
Joined
Jan 8, 2015
Posts
102
Reaction score
30
Ni furaha kwa wazee wastaafu Wilaya ya Same kuzindua rasmi umoja wao.

Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Same ambapo Mkuu wa Wilaya ya Same Mh. Rosemaey Senyamule alikuwa ni mgeni Rasmi.

Lengo la umoja ni pamoja Na kushirikishana fursa Na kutatua matatizo yanayowakabili, ikiwemo madai ya mafao kwa wanaochelewa kupata mafao yao.

DC huyo alitoa wito kwao watumie uzoefu wao kuelimisha vijana. Kwani wana hazina kubwa ya maarifa.

Pia waone namna ya kuimarisha umoja huo kikata kwani ni rahisi kukutana kuliko Wilaya.

Aliwaeleza Juu ya utaratibu wa serikali wa kuwapa matibabu bure wazee wasiojiweza. Na kutenga dirisha la wazee kwenye vituo vya Huduma za Afya.

Aliwaagiza idara ya maendeleo/ ustawi wa jamii. Kuwa Karibu Na wazee Na kujua shida zao Na kuzitatua kwa wakati.

Kwa Takwimu, Wilaya ya Same inaongoza kuwa Na wazee wengi zaidi ( zaidi ya 15000). Kulinganisha Na Wilaya nyingine za Tanzania.

Kivutio ilikuwa ni mzee Mwenye miaka 92 aliyekuwa akurukaruka kwa furaha baada ya uzinduzi huo.

" Wazee wangu Naomba mfundishe kinachowafanya kuishi muda mrefu mkiwa Na nguvu zenu" Hayo yalisemwa Na Mkuu wa Wilaya ya Same ,mh Rosemary Senyamule baada ya uzinduzi wa umoja huo. Uliofanyika tar. 06/08/2017.
 
IMG-20170822-WA0002.jpg
DC MH: ROSEMARY SENYAMLE AKIWA NA WAZEE WASTAAFU.

IMG-20170822-WA0001.jpg

DC AKIONGEA NA WAZEE WASTAAFU
 
Ni furaha kwa wazee wastaafu Wilaya ya Same kuzindua rasmi umoja wao.

Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Same ambapo Mkuu wa Wilaya ya Same Mh. Rosemaey Senyamule alikuwa ni mgeni Rasmi.

Lengo la umoja ni pamoja Na kushirikishana fursa Na kutatua matatizo yanayowakabili, ikiwemo madai ya mafao kwa wanaochelewa kupata mafao yao.

DC huyo alitoa wito kwao watumie uzoefu wao kuelimisha vijana. Kwani wana hazina kubwa ya maarifa.

Pia waone namna ya kuimarisha umoja huo kikata kwani ni rahisi kukutana kuliko Wilaya.

Aliwaeleza Juu ya utaratibu wa serikali wa kuwapa matibabu bure wazee wasiojiweza. Na kutenga dirisha la wazee kwenye vituo vya Huduma za Afya.

Aliwaagiza idara ya maendeleo/ ustawi wa jamii. Kuwa Karibu Na wazee Na kujua shida zao Na kuzitatua kwa wakati.

Kwa Takwimu, Wilaya ya Same inaongoza kuwa Na wazee wengi zaidi ( zaidi ya 15000). Kulinganisha Na Wilaya nyingine za Tanzania.

Kivutio ilikuwa ni mzee Mwenye miaka 92 aliyekuwa akurukaruka kwa furaha baada ya uzinduzi huo.

" Wazee wangu Naomba mfundishe kinachowafanya kuishi muda mrefu mkiwa Na nguvu zenu" Hayo yalisemwa Na Mkuu wa Wilaya ya Same ,mh Rosemary Senyamule baada ya uzinduzi wa umoja huo. Uliofanyika tar. 06/08/2017.
Ndugu yangu nimetupiamo picha hizo nilitumiwa na Mzee wangu anayevutiwa na utendaji wa huyu Mama mko naye hapo
 
Hizo ndio kazi za kiongozi sio ujinga wa Tarime,Hai na Dar
 
Back
Top Bottom