GE2025 DC Mkude: Hakuna atakayeandamana Arusha

GE2025 DC Mkude: Hakuna atakayeandamana Arusha

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude, amewatoa hofu wananchi wa Arusha kuhusu hali ya usalama katika jiji hilo kuelekea zoezi la upigaji kura linalotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

Akizungumza leo Oktoba 27, 2025, ofisini kwake, Mkude amesema Jeshi la Polisi limejipanga vyema kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa amani na utulivu. Amesema Ofisi yake imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha usalama, ikiwemo kuzungumza na vijana, wazee, wanawake pamoja na wagombea wa vyama vya siasa, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano na kudumisha amani kuelekea uchaguzi huo.

Mkude ameongeza kuwa kutokana na maandalizi yaliyofanyika, hana shaka kuwa hakutakuwepo na maandamano yoyote katika Jiji la Arusha siku ya upigaji kura, licha ya kuwepo kwa taarifa za upotoshaji mitandaoni.

“Nimekuwa nikisikia taarifa mtandaoni zikidai kuwa kutakuwa na maandamano, lakini niwahakikishie wananchi kuwa hali ya usalama ipo shwari na hakuna tukio kama hilo litakalotokea,” amesema Mkude.

Aidha, amewataka wananchi wa Arusha kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la upigaji kura, akiwahakikishia kuwa ulinzi utaimarishwa kikamilifu katika maeneo yote ya jiji.
 
Back
Top Bottom