PreGE2025 DC Kiswaga: Endapo William Lukuvi atagoma kustaafu Ubunge Isimani, wananchi tutamstaafisha kwa lazima

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
79,080
Reaction score
84,967
Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Festo Kiswaga, ametangaza rasmi nia yake ya kugombea ubunge katika Jimbo la Isimani, mkoani Iringa, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Lumilo Hotel, Manispaa ya Iringa, Kiswaga amesema kuwa uamuzi huo umetokana na wito wa wananchi wa Isimani na nafasi iliyojitokeza baada ya Mbunge wa sasa, Mhe. William Lukuvi, kutangaza mwaka 2020 kuwa hatogombea tena ifikapo uchaguzi wa mwaka huu.

“Nina dhamira ya dhati kulitumikia Jimbo la Isimani. Mheshimiwa Lukuvi mwenyewe alitangaza kuwa hatagombea tena mwaka 2025, na ninasimama kwa ujasiri mkubwa kuchukua kijiti na kuendeleza maendeleo,” alisema Kiswaga mbele ya waandishi wa habari.

Akiendelea kufafanua, Kiswaga alisema kuwa mwaka 2022 aliitwa na Lukuvi jijini Dodoma, ambapo walizungumza kwa kina, na Lukuvi alimueleza kuwa amehudumu kwa zaidi ya miaka 30 na hatakuwa tena kwenye kinyang’anyiro cha ubunge.

“Kama ni kweli kwamba anapenda maendeleo ya Jimbo hili, basi kwa maslahi mapana ya wananchi wa Isimani, ni vyema akaheshimu kauli yake na kustaafu kwa hiari. Vinginevyo, wananchi wamesema wako tayari kumstaafisha kwa lazima kupitia sanduku la kura,” aliongeza Kiswaga.

vijana mumewekewa mazingira ya ajira, bbt, madereva wa omani, ajira tra jeshi police, bado na ubunge mnataka simkalime, basi anzeni kuwakata panga wazee kama kule meatu
 
Huyu lukuvi alishawahi kuwa mbunge na mkuu wa mkoa kwa wakati mmoja.
Ni yeye aliyemshika JPM mkono kisha akaishia kuukwaa uwazir wa ardhi na nyumba.
Yaani jambazi unampa wizara ya ardhi
 
Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Festo Kiswaga, ametangaza rasmi nia yake ya kugombea ubunge katika Jimbo la Isimani, mkoani Iringa, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Lumilo Hotel, Manispaa ya Iringa, Kiswaga amesema kuwa uamuzi huo umetokana na wito wa wananchi wa Isimani na nafasi iliyojitokeza baada ya Mbunge wa sasa, Mhe. William Lukuvi, kutangaza mwaka 2020 kuwa hatogombea tena ifikapo uchaguzi wa mwaka huu.

“Nina dhamira ya dhati kulitumikia Jimbo la Isimani. Mheshimiwa Lukuvi mwenyewe alitangaza kuwa hatagombea tena mwaka 2025, na ninasimama kwa ujasiri mkubwa kuchukua kijiti na kuendeleza maendeleo,” alisema Kiswaga mbele ya waandishi wa habari.

Akiendelea kufafanua, Kiswaga alisema kuwa mwaka 2022 aliitwa na Lukuvi jijini Dodoma, ambapo walizungumza kwa kina, na Lukuvi alimueleza kuwa amehudumu kwa zaidi ya miaka 30 na hatakuwa tena kwenye kinyang’anyiro cha ubunge.

“Kama ni kweli kwamba anapenda maendeleo ya Jimbo hili, basi kwa maslahi mapana ya wananchi wa Isimani, ni vyema akaheshimu kauli yake na kustaafu kwa hiari. Vinginevyo, wananchi wamesema wako tayari kumstaafisha kwa lazima kupitia sanduku la kura,” aliongeza Kiswaga.

View attachment 3354666
Kila laheri Festo..
 
Back
Top Bottom