DC Kinondoni tusaidie tupate silaha zetu

mluhilamkuu

Member
Dec 8, 2014
50
25
Kwanza nikupongeze kwa kuaminiwa na Mh. Rais mpaka kufikia hatua ya kukuteua kumuwakilisha. Pili nikupongeze kwa kasi nzuri uliyoanza nayo ambayo kwa namna moja au nyingine inaendana na kasi ya Mh.Rais.

Nikiwa kama mkazi wa Wilaya yako ya Kinondoni, naandika ujumbe huu nikiwa na masikitiko makubwa. Nimejikongoja na kujenga kibanda changu cha kuishi huko Kibamba. Tatizo ninalokabiliana nalo mimi na wakazi wengi wa huko ni ongezeko la uhalifu. Suala la kuvamiwa, kujeruhiwa na kuibiwa mali zetu tunazozipata kwa kuvuja jasho limekithiri sana.

Na heri wahalifu hao wangekuwa wanaishia kutujeruhi ma kutuibia tu, lakini wamevuka mipaka mpaka kufikia hatua ya kuwaweka chini ya ulinzi wakaaji wote wanaowakuta kwenye nyumba husika waliyoivamia, wanawavua nguo wote na kubaki uchi wa mnyama, kisha wanaanza kuwaingilia wote mmoja baada ya mwingine uwe mwanaume au mwanamke. Kwa hiyo wanaweza kukufanya wewe baba, mama,watoto wako, house girl, kama mama mkwe kaja kukutembelea nae wanamfanya na yeyote anayekuwepo nyumbani wakati huo, kisha wanatokomea kusikojulikana.

Lakini sikitiko kubwa zaidi ni kwamba binafsi nilijichanga nikanunua silaha ndogo (Bastola) pale duka la Tanganyika Arms ili inisaidia kujihami. Lakini tangu nilipoinunua mwezi January 2014 mpaka leo bado sijapewa kibali cha umiliki licha ya kukamilisha hatua zote na file limekwama hapo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Nilishapigiwa simu mara tatu kwa nyakati tofauti na Ofisi yako ili nije kuhudhuria bila kukosa kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama cha Wilaya kinachotakiwa kujadili maombi yangu ya kumiliki silaha lakini mara zote tatu nimekuwa nikifika na kuwakuta waombaji wenzangu wengine, tunakalishwa hapo masaa manne kisha tunaambiwa Mkuu wa Wilaya ana udhuru hivyo tuondoke tutawapigiwa simu siku nyingine.

Hii imetokea mara tatu mara ya mwisho ikiwa mwezi February mwaka huu. Na toka hapo sijapigiwa simu tena licha ya mimi kupiga simu mara kwa mara hapo Ofsini kwako kuulizia na kujibiwa kwamba kikao bado hakijaitishwa. Mh. Makonda ameondoka, naomba basi wewe tusaidie maana silaha yangu kwa mfano niliinunua tsh 3,300,000 hivyo tangu January 2014 mpaka sasa ni miaka miwili na miezi minne, silaha imekaa tu kule dukani huku mtaani tunajeruhiwa, kubakwa na wengine kufanywa kinyume na maumbile, ni haki kweli hii?Maana naamini hiyo pesa ningekuwa nimeizungusha hata kwa kuuza karanga kwa muda huu wa miaka miwili ingekuwa imezaa!!!

Na kule dukani Tanganyika Arms si kwamba inakaa bure, nitakapoenda kuichukua baada ya kubata kibali (sijui itakuwa lini)lazima watanitaka nilipe gharama za utunzaji maana wao wanahesabu mwaka mmoja ndio naihifadhi bure, baada ya hapo natakiwa kulipia kila siku silaha inapokaa kule kanakwamba mimi ndie niliyechelewa kwa makusudi kwenda kuichukua!!!

Naomba tusaidie kwa hilo Mh. Mkuu wa Wilaya, kubakwa kwa wanawake au kugeuzwa na kufanywa kwetu wanaume ni jambo baya sana. Mafaili yapo hapo Ofisini kwako tunazungushwa tu mwaka wa pili na nusu sasa. Hivi kuna ugumu gani wa kuitisha Kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama cha Wilaya kutujadili ili mafaili yaende Mkoani?Kila siku Mh. Makonda alikuwa ana udhuru, basi kwa niaba ya waombaji wengine ambao mafaili yao yamekwama hapo Wilayani tunaomba utusaidie uhitishe kikao husika.

Wako katika Ujenzi wa Tanzania Mpya
 
Heshima kwako! Ni kweli nami nina jamaa zangu 3 wote walinunua 2014 hadi sasa vibali havijatoka! Nasikia RC Makonda amejipenyeza nae awe ana sign vibali vya silaha...sijajua vya Tanzania nzima vinavyoombewa Makao Makuu au kwa wa Dar pekeyao! Urasimu umeongezeka mara dufu: Pole kwa usumbufu mkuu!! Vumilia na fuatilia zaidi na zaidi bil kuchoka

Back
Top Bottom