DC Kinondoni amaliza tatizo la Madawati

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi amemaliza agizo la Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli la kuhakikisha kero ya upungufu wa madawati inamalizwa.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari wakati wa maswali na majibu katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam baada ya kula kiapo cha utii, Hapi alimueleza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuwa ikiwa ni siku yake ya 74 tangu kuteuliwa kushika wadhifa huo, amemaliza tatizo la madawati.
"Tulikua na upungufu wa madawati zaidi ya 30,800 Kinondoni. Hii ilikua ni zaidi ya 50% ya ya upungufu wa madawati wa mkoa mzima wa Dar es salaam. Lakini ninayo fahari kukufahamisha kuwa tumemaliza changamoto hiyo kwa asilimia 100."

Mkuu huyo wa wilaya alimuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kumruhusu kutumia mgao wa pesa za harambee zinazoendelea kukusanywa na Mkuu wa mkoa katika kukabiliana na tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa.

"Baada ya kumaliza changamoto ya madawati, tumejipanga kuanza kushughulikia upungufu wa vyumba vya madarasa. Maana tunaamini baadhi ya madawati yanayoendelea kutengenezwa yatakosa mahali pa kuyaweka. Tunao upungufu wa vyumba vya madarasa zaidi ya 1800 ambavyo tunapaswa kujenga. Tunaomba mgao wetu wa ziada wa michango ya madawati tuutumie kujenga madarasa..." alisema Mh. Hapi.

Wakuu wa wilaya wa Dar es salaam wamekula kiapo cha uaminifu jana mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda. Waliokula kiapo ni Mh. Sofia Mjema wa Ilala, Mh. Felix wa Temeke, Mh. Hashim Mgandilwa wa Kigamboni na Mh. Ally Hapi wa Kinondoni. Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Humphrey Polepole hakuwepo kutokana na udhuru.
fa7c5979f1331fb38727ce3227babf0f.jpg
 
Makonda kachangia kiasi gani? mi nimechanga 50000 Make Cheo ni dhamana tu! pia wilaya ambazo hazijafikia malengo wakurugenzi wa ccm wawajibishwe! ndo wafuja ela za maendeleo Kwa kujilipa posho! mfano! mwezi wa 2-3 tumeona mkuu wa Mkoa moro kulalamika kulipa hewa zaid ya bil. 1. 2 ktk almashauri
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Back
Top Bottom