Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,411
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi
Kwa ufupigo lake ni kuhakikisha kwamba Kinondoni yenye shule za msingi 140 ndani ya kipindi kifupi inaondokana na tatizo la watoto kukaa chini, ili kuinua taaluma katika manispaa hiyo.
Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi amesema Shule za msingi Manispaa ya Kinondoni zinakabiliwa na upungufu wa madawati 19,386, vyumba vya madarasa 2,235 na matundu ya vyoo 6,788, huku akitoa rai kwa mashirika na sekta binafsi kusaidia kutatua kero hiyo.
Amesema lengo lake ni kuhakikisha kwamba Kinondoni yenye shule za msingi 140 ndani ya kipindi kifupi inaondokana na tatizo la watoto kukaa chini, ili kuinua taaluma katika manispaa hiyo.
Hapi ameyasema hayo leo alipokuwa akipokea msaada wa madawati ya kisasa 124 uliotolewa kwa udhamini wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, kwa ajili ya Shule ya Msingi Nakasangwe.
Amesema shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 1,385 awali ilikuwa na madawati 60 pekee hivyo msaada huo utapunguza idadi ya wanafunzi waliokuwa wakikaa chini.
“Ni wazi kwamba serikali ina wajibu wa kutekelewa mapungufu haya ya elimu bure, lakini natoa rai kwa mashirika mbalimbali, sekta binafsi na wafanyabiashara kujitokeza kutoa msaada kwa serikali ili kutekeleza sera ya elimu bure iliyoletwa na Rais wetu, Dk Magufuli,” amesema Hapi.
Akikabidhi msaada huo Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe amesema jamii inapaswa kuingilia kati ili kujitolea kwani nguvu ya serikali pekee haitoshi.
“Serikali ya awamu ya tano ilikuja na sera ya elimu bure, watoto wengi wameandikishwa shule, awali wengi walibaki majumbani lakini changamoto ikaibuka ambayo ni pamoja na madawati, watoto wengi wanakaa chini, LAPF inakuza wanachama wake wa baadaye tumetoa madawati ili watoto hawa ambao ndiyo wajenzi wa taifa baadaye waweze kusoma katika hali ya utulivu,” amesema Mlowe.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Kiduma Mageni amesema Manispaa hiyo yenye jumla ya wanafunzi 169,388 bado inakabiliwa na changamoto ya madawati, huku baadhi ya wanafunzi wakikaa chini.
Chanzo: Mwananchi