Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 875
- 960
Akiwa na siku 85 tangu kuchaguliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni 21/April/2016 Ally Salum Hapi ameendelea kutekeleza kwa vitendo majukumu aliyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais John Pombe Magufuli.
Licha ya kusimamia suala la watumishi hewa katika wilaya yake ambao walikuwa 34 na kufikia 101, huku akisimamia vyema na Kulimaliza suala la upatikanaji wa madawati katika wilaya yake ambapo imekuwa changamoto kubwa tangu kutangazwa kwa Elimu bure.
Mkuu wa Wilaya Ally Salum Hapi ameelendelea na kasi hiyo ya HAPA KAZI TU ambapo siku ya leo ametembelea maeneo ya Tandale Hospitali, Uwanja wa Fisi na Soko la Tandale kwa ajili ya kusikiliza kero za wakazi wa maeneo hayo.
Akizungumza na wakazi hao amewataka kuzingatia suala la usafi na kuhakikisha wanakuwa na vifaa vya kuwekea uchafu katika maeneo yao huku akiwasisitiza wale wenye sehemu za kuegeshea magari katika maeneo yao kuyaweka katika mazingira ambayo hayataleta athari