Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 875
- 960
Kanisa la The Pool of Silome Church wametoa mchango wa Shilingi Milioni 19 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi ikiwa ni mchango wao wa Madawati kwa wilaya hiyo.
Akikabidhi mchango huo kwa niaba ya waumini wa kanisa hilo Mchungaji Elia amesema waumini wake wameguswa sana na tatizo la madawati kwenye wilaya ya Kindondoni ndiyo maana wameamua kuchanga pesa hizo.
Hafla hiyo iliyofanyika saa saba mchana kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ilihudhuriwa na Mchungaji Eliah akiwa na waumini wake wakiwa wamevalia nguo zao nyeupe kama ishara ya upendo kwa watu wote.
Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni, RPC Kinondoni na katibu tawala wa wilaya ya Kinondoni.Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Ally Hapi aliwashukuru waumini wa kanisa hilo na kuziomba taasisi nyingine ziige mfano huo kwa kuchangia madawati zaidi katika wilaya hiyo ya Kinondoni.