DC Hapi afungua mafunzo ya ujasiriamali awamu ya pili kwa vijana 2000 wa Kinondoni

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
DC HAPI AFUNGUA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI AWAMU YA PILI KWA VIJANA 2000 WA KINONDONI

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Ally Hapi leo tarehe 07/12/2016 amefungua rasmi mafunzo ya ujasiliamali kwa awamu ya pili wilayani Kinondoni.

Katika Uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya amewata Vijana kuondokana na mawazo ya kuajiriwa pindi wanapohitimu vyuo vya Elimu ya juu na hata wale wasio na elimu hiyo, bali wajikite kutumia fursa zilizopo kujiajiri jambo ambalo litawasaidia kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira na kujenga uchumi wao na wa taifa.
"Kazi tunayoifanya hapa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, ambayo inaeleza wazi katika ukurasa wa 115 na kuendelea kuwa jukumu la serikali ya awamu ya Tano ni kuwasaidia vijana wa elimu tofauti kujiajiri na kufanya shughuli za ujasiriamali katika vikundi. Tunaendelea na awamu hii ya pili itakayonufaisha vijana elfu mbili, na tutaendelea na awamu nyingine hadi tumalize vijana wote elfu kumi waliojiandikisha."
Alisema Hapi.

DC Hapi amesema ameanzisha mafunzo hayo kwa nia ya kuwaondoa uwoga vijana na kuwajengea ujasiri na uthubutu katika kuamua kujiajiri kwani amebaini vijana wengi na hasa wanaohitimu vyuoni ni wazito na waoga kujiajiri, jambo ambalo ameeleza kuwa linatokana na mfumo wa elimu kujikita katika nadharia zaidi kuliko kuwaandaa vijana kifikra na kivitendo kuanzisha shughuli zao binafsi za kiuchumi.

Vijana ambao wameanza mafunzo hayo leo wamemshukuru Mkuu huyo wa wilaya huku wakiahidi kuitumia elimu watakayopewa kujenga maisha yao na uchumi wa taifa.

Vijana wapatao 10,000 walijitokeza kuitikia wito wa kampeni iliyoanzishwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni mapema mwezi June ambao watapatiwa mafunzo ya ujasiriamali bure ili kujiandaa kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira nchini.
Awamu hii ya mafunzo inajumuisha washiriki 2000 kwa uwakilishi kutoka kila kata katika kata 20 za Kinondoni.

Hapi alisisitiza kuwa ndoto yake ni kuona uongozi wake unagusa maisha ya watu wanyonge na kwamba anaamini ndoto hiyo itatimia.
"Wale wanaodhani tulitoa ahadi hewa wanathibitisha leo, wale wanaofikiri tutashindwa napenda kuwahakikishia kuwa kwa uwezo wa Mwenyeezi Mungu ndoto hii itatimia na wananchi wote elfu kumi watapewa mafunzo bure."
Alisema DC Hapi.

Mafunzo hayo yamefunguliwa katika ukumbi wa King Solomon Namanga jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka benki ya NMB, Shirika la PPF, Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi pamoja Balozi wa heshima wa Sierre lione nchini.
1481125001573.jpg
 
Hii kitu nimeipenda! Nina kijana wangu,Mungu akimjalia anamaliza Chuo kikuu mwaka kesho,natamani tungeishi Kinondoni ili ameze hii kitu.
 
Vijana wa CHADEMA nao wafundishwe kujiajiri waache kulalamika hawana mitaji wakati muda wote wanashinda mitandaoni kuibeza serikali
 
Hii kitu nimeipenda! Nina kijana wangu,Mungu akimjalia anamaliza Chuo kikuu mwaka kesho,natamani tungeishi Kinondoni ili ameze hii kitu.
Safi sana Mpangishie geto tu kinondoni tayari anakua mkazi wa kinondoni Jumla
 
Amenifurahisha kitu kimoja kwamba ukitaka utajiri huwezi kuupata kwa kuajiriwa
 
Kama niliweza Kufaulu Financial Management, Management Accounting, Corporate Finance, Entreprenurship, Taxation, Public Finance, yalikua na Mchango kwangu sioni Kama seminar za Kisiasa kama zitamsaidia mtu kama kichwa kingesomeka Ali hapi awapata mitaji Vijana 2000 ningepongeza lakini kujitengenezea Per diem kwa kuwarudisha watu Darasani. Disgusting!
 
Ni kwamba kata yangu WEO hajielewi au? Sikusikia hata mchakato wa kumtafuta mwakilishi kutoka kata niliyopo, au jina limeuzwa?
 
Hongera sana DC hapi nategemea maDC wengine watafuata Mfano wako.kaza boti Hapi
 
Kama niliweza Kufaulu Financial Management, Management Accounting, Corporate Finance, Entreprenurship, Taxation, Public Finance, yalikua na Mchango kwangu sioni Kama seminar za Kisiasa kama zitamsaidia mtu kama kichwa kingesomeka Ali hapi awapata mitaji Vijana 2000 ningepongeza lakini kujitengenezea Per diem kwa kuwarudisha watu Darasani. Disgusting!

GP kama kweli ulisomeya hayo ulio orodhesha Basi wasomi hatuna.Hivi mitaji NI nini ?.wapo watu wengi wana pesa Lakini hawana mitaji ya akili Na wako watu wengi wenye akili hawana mitaji ya pesa.Hizo semina zinawakutanisha hao wawili.
Kutokana Na usomi wako ungeweza kutuelimisha sio unaleta usiasa.
 
Acha kutuletea akili Za Vijiweni Akili si Mtaji
 
GP kama kweli ulisomeya hayo ulio orodhesha Basi wasomi hatuna.Hivi mitaji NI nini ?.wapo watu wengi wana pesa Lakini hawana mitaji ya akili Na wako watu wengi wenye akili hawana mitaji ya pesa.Hizo semina zinawakutanisha hao wawili.
Kutokana Na usomi wako ungeweza kutuelimisha sio unaleta usiasa.
MTU anakuambia Nina m 20 lakini sijui biashara ya kufanya!
 
Mkuu Mbona wako wengi tu.Huwezi ambiwa Nina M20 Ila atakupa mbegu ukiipanda badala ya kuila hizo M 20 zitakuwa juu ya meza.
UAMINIFU UAMINIFU UAMINIFU.
Watu wengi wenye pesa wameishia BAKORA(la saba) Na wengine la nne
 
DC HAPI AFUNGUA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI AWAMU YA PILI KWA VIJANA 2000 WA KINONDONI

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Ally Hapi leo tarehe 07/12/2016 amefungua rasmi mafunzo ya ujasiliamali kwa awamu ya pili wilayani Kinondoni.

Katika Uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya amewata Vijana kuondokana na mawazo ya kuajiriwa pindi wanapohitimu vyuo vya Elimu ya juu na hata wale wasio na elimu hiyo, bali wajikite kutumia fursa zilizopo kujiajiri jambo ambalo litawasaidia kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira na kujenga uchumi wao na wa taifa.
"Kazi tunayoifanya hapa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, ambayo inaeleza wazi katika ukurasa wa 115 na kuendelea kuwa jukumu la serikali ya awamu ya Tano ni kuwasaidia vijana wa elimu tofauti kujiajiri na kufanya shughuli za ujasiriamali katika vikundi. Tunaendelea na awamu hii ya pili itakayonufaisha vijana elfu mbili, na tutaendelea na awamu nyingine hadi tumalize vijana wote elfu kumi waliojiandikisha."
Alisema Hapi.

DC Hapi amesema ameanzisha mafunzo hayo kwa nia ya kuwaondoa uwoga vijana na kuwajengea ujasiri na uthubutu katika kuamua kujiajiri kwani amebaini vijana wengi na hasa wanaohitimu vyuoni ni wazito na waoga kujiajiri, jambo ambalo ameeleza kuwa linatokana na mfumo wa elimu kujikita katika nadharia zaidi kuliko kuwaandaa vijana kifikra na kivitendo kuanzisha shughuli zao binafsi za kiuchumi.

Vijana ambao wameanza mafunzo hayo leo wamemshukuru Mkuu huyo wa wilaya huku wakiahidi kuitumia elimu watakayopewa kujenga maisha yao na uchumi wa taifa.

Vijana wapatao 10,000 walijitokeza kuitikia wito wa kampeni iliyoanzishwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni mapema mwezi June ambao watapatiwa mafunzo ya ujasiriamali bure ili kujiandaa kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira nchini.
Awamu hii ya mafunzo inajumuisha washiriki 2000 kwa uwakilishi kutoka kila kata katika kata 20 za Kinondoni.

Hapi alisisitiza kuwa ndoto yake ni kuona uongozi wake unagusa maisha ya watu wanyonge na kwamba anaamini ndoto hiyo itatimia.
"Wale wanaodhani tulitoa ahadi hewa wanathibitisha leo, wale wanaofikiri tutashindwa napenda kuwahakikishia kuwa kwa uwezo wa Mwenyeezi Mungu ndoto hii itatimia na wananchi wote elfu kumi watapewa mafunzo bure."
Alisema DC Hapi.

Mafunzo hayo yamefunguliwa katika ukumbi wa King Solomon Namanga jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka benki ya NMB, Shirika la PPF, Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi pamoja Balozi wa heshima wa Sierre lione nchini.
View attachment 443593
Ukitambulisha aliyeandika hii thread una ban
 
Back
Top Bottom