mende 2014
JF-Expert Member
- Apr 13, 2014
- 763
- 131
Mkuu wa wilaya ya Bunda Mh. Joshua Mirumbe awa mbogo kwa Polisi katika kikao kilichofanyika hapa Bunda katika mtaa wa Mapinduzi kujadili wizi wa kutumia silaha za moto unaotokea mara kwa mara katika mji huu.
Wananchi waliilalimikia jeshi la Polisi kutofika kwenye tukio kwa wakati licha ya kupewa taarifa mapema. Pia walisema kuwa wakienda Polisi wanapewa majibu mabaya ambayo hayaendana na utendaji wa kazi.
Baada ya Mkuu wa wilaya kuridhishishwa na maelezo hayo likiwemo tukio la usiku wa saa tisa kuamkia leo ambapo DC aliwapigia Simu Polisi lakini bado wakachelewa kufika, aliwapa siku 4 wahakikishe Bunduki iliyofanya tukio ipatikane tofauti na hapo hawafai kuwa katika wilaya hii.
Wanachi walisema hamhitaji OCD na OCS maana matukio yanafanyika kila leo na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na Polisi ikionyesha kuwa wao nao ni wezi. Wananchi walisema kipindi cha peter ouma (OCD) na Mayunga (OCS) wananchi walikaa kwa amani sana sasa iweje walipotoka na kuletwa wengine matukio yanazidi?
Pamoja na hayo , katika kikao hicho OCCID & OCS ndio walikuwepo na OCS akiwa amechelewa kufika lakini OCD hakufika kabisa. OCCID ni Mgeni ana siku nne ambapo tukio la leo ndilo limemkuta hapa na amesema tayari mtu mmoja ameishakamatwa na pia amewahakikishia wananchi kuwa wawe na imani naye atafanya kazi kwa bidii na kuhakikisha hiyo hali inaisha na endapo hatafanya kazi basi wananchi wamshitaki kwa DC. Kwa ujumla wananchi walikasirika sana.

Last edited by a moderator: